HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 26, 2018

TAKUKURU PWANI YAMFIKISHA MAHAKAMANI MTUMISHI DAWASA KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Pwani, imemfikisha mahakamani Romani Michael Jovin ambae ni  (volunteer surveyor )wa DAWASA kwa kosa la kuomba rushwa ya sh.70,000  na kupokea  ya kiasi cha sh.50,000 .

Mtuhumiwa huyo amejikuta akifikishwa kizimbani baada ya kwenda kinyume na kifungu cha 15(1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba. 11 ya mwaka 2007. Romani Michael ambaye alifunguliwa kesi ya jinai mamba 140 ya mwaka 2018 ni volunteer Surveyor DAWASA Ubungo.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu mkazi wilaya ya Kibaha  Herieth Mwailolo, mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Prisca Mpeka amedai,   mshitakiwa alitenda kosa la kuomba rushwa ya sh.70,000 na kupokea rushwa ya sh. 50,000 kutoka kwa mtoa taarifa  ili aweze kumsaidia mtoa taarifa kupata mita ya DAWASA.

Alidai  jambo hilo ni kosa kisheria kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, sheria namba 11 ya mwaka 2007.

Aidha Prisca alidai , mshitakiwa alipokea rushwa ya kiasi cha sh.50,000 kutoka kwa mtoa taarifa, jambo ambalo pia ni kosa kisheria  kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa, namba 11 ya mwaka 2007. 

Mshitakiwa alikana makosa yote mawili na amerudihswa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 27/11/2018.

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Pwani, Suzana Raymond anaendelea kuwaasa wananchi wote kufuata taratibu kanuni na sheria za nchi ili kuweza kwenda na kasi ya awamu ya tano chini ya Raisi dk. John Magufuli.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad