HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 26, 2018

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN AHUDHURIA MKUTANO WA BLUE ECONOMY KENYA LEO

 RAIS wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Uchumi Endelevu wa Bahari (Sustainable Blue Economy Conference) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi Nchini Kenya leo 26/11/2018 na kuwashirikisha Marais mbalimbali wa Nchi za Afrika.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa kuhusiana na Uchumi Endelevu wa Bahari (Sustainable Blue Economy Conference ) uliofanyika katika ukumbi wa Kmataifa wa mikutano wa Kenyatta, akiwasilisha Tamko la Serikala ya Jamuhuri ya Muungano, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli.katika mkutano huo uliofanyika leo 26/11/2018, jijini Nairobi Kenya.
 BAADHI ya Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa Unaozungumzia Uchumi Endelelevu wa Bahari (Sustainable Blue Economy Conference) uliofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kanyatta Jijini Nairobi Kenya, leo 26/11/2018. Wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Mkutano huo akitowa Tamko la Serikali ya Jamuhuri ya Muungano, akimuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Monica Juma, alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Sustainable Blue Economy).
 BAADHI ya Washiriki kutoka Nchini mbalimbali wakiwasili katika viwanja vya Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi kuhudhuria Mkutano wa Uchumi Endelevu wa Bahari.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad