HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 15 November 2018

MIUNDOMBINU YA RELI YABORESWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO- KADOGOSA

Na Khadija Seif,globu ya jamii

Shirika la reli nchini (TRC) katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli wameboresha sekta ya Miundombinu ya reli pamoja na kujenga reli ya kisasa "standard Gauge Railways " (SGR).

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa shirika la reli nchini(TRC) Masanja Kungu Kadogosa amesema shirika hilo lina majukumu ya kutoa huduma za usafiri wa abiria wa treni za mikoani pamoja na treni za mizigo ndani ya nchi na nje ya nchi.

Amesema kwa sasa TRC imerudisha safari ya treni ya mizigo kutoka Dar es salaam mpaka Mji wa Kampala nchini Uganda, ambapo ikiwa na miradi miwili ambayo ni Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na Mradi wa uboreshaji wa reli ya kati pamoja na Miradi midogo kama kurejesha njia ya Tanga,Arusha na Moshi na baadae Mtwara,Mbambabei na njia ya Singida.

Na Kadogosa amefafanua zaidi kuwa Mapato yameongezeka kutokana na huduma zinazotolewa na TRC na kuboreshwa kwa huduma za shirika kwa mwaka 2017/2018 na kufikia kiasi cha bilioni 36 tofauti na mwaka 2016/2017 ambapo kiasi cha pesa kilikua bilioni 23.

Aidha, ameeleza Mradi unaendelea kutekelezwa katika sehemu mbili za mwanzo zinazojumuisha Dar es salaam,Makutopora kwa lengo la ifikapo 2021 mwezi wa pili , sehemu hizi mbili za Mradi ziwe zimekamilika. 

Na katika ujenzi huo shirika la reli (TRC) limetoa tenda kwa wakandarasi ambao ni ubia wa kampuni ya Yapi Merkezi kutoka nchi ya Uturuki na Mota Engil kutoka Ureno.

Sanjari na hilo kuna Kampuni za wazawa 16 zinazoshiriki katika ujenzi wa reli ya kisasa kama Wakandarasi,Wasambazaji wa bidhaa na watoa huduma, lengo likiwa ni kushirikiana kati ya wazawa na wageni katika kujifunza na kujiongezea ufanisi mkubwa ili kuleta maendeleo Kwenye nchini yetu hususani Kwenye usafiri wa treni amesema Kadogosa.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Reli (TRC) 
Masanja Kungu Kadogosa  
akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akitoa taarifa kuhusu maboresho yaliyofanywa pamoja Miundombinu ya Reli Katika miaka mitatu ya serikali ya awamu ya tano

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad