HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 15 November 2018

DSTV YAZINDUA KAMPENI MPYA YA SIKUKUU 'NI MUDA WA KUKIWASHA NA DSTV'

  Na Khadija seif,globu ya jamii
KAMPUNI  ya MultiChoice Tanzania imetangaza ofa Kabambe kwa wateja wake na  kwa wale wanaojiunga na huduma zao kupitia kampeni yake maalum inayokwenda kwa jina la  "Ni muda wa Kukiwasha na DSTV."

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo,Meneja Masoko wa kampuni ya MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema wateja wao sasa watapata burudani zaidi za kusisimua kupitia soka,filamu,Tamthilia,Katuni na vipindi mbalimbali vya watoto vitakavyoiletea familia pamoja na kuimarisha upendo.

Aidha Mria ameeleza kuwa mara kwa mara wamekuwa wakiwatunuku wateja wao wa zamani na wapya zawadi na ofa Kabambe huku wakiendelea kupata burudani ya uhakika muda wote kwani kwa mwaka huu wamekua wakitoa mfululizo wa zawadi kwa wateja wote.

Kwa upande wa Mkuu wa Mauzo wa Kampuni hiyo Salum Salum amefafanua ofa hiyo ni zawadi ya kufunga mwaka kwa wateja wapya wa Dstv kwani katika kipindi cha miezi miwili wataweza kuunganishwa kwa gharama ya shilingi elfu 79 tu  na kupewa kifurushi cha Bomba cha mwezi mmoja bila malipo ya ziada.


 Vilevile mbali na kuongezwa kwa chaneli na maudhui kedekede kwa wateja pia kwa wale ambao hawajajiunga hawajasahauliwa na kwa sasa watapata ofa hiyo Kabambe ya Kujiunga kwa gharama nafuu zaidi ya hapo wapate kifurushi cha mwezi mmoja bila malipo ambayo ni zawadi ya sikukuu kwa wateja wetu alisema Salum Salum .

 Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Ni muda mzuri Kukiwasha na DSTV   utakaowapa fursa wateja wao kupata burudani zaidi za kusisimua kupitia soka,filamu,Tamthilia,Katuni na vipindi mbalimbali vya watoto vitakavyoiletea familia pamoja na kuimarisha upendo.
 Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania Salum Salum akifafanua kuhusu ofa hiyo Kabambe msimu huu wa sikukuu  itakayowapa fursa wateja wao kupata burudani zaidi za kusisimua kupitia soka,filamu,Tamthilia,Katuni na vipindi mbalimbali vya watoto vitakavyoiletea familia pamoja na kuimarisha upendo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad