HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 28 November 2018

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB, IKULU JIJINI DAR LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyemtembelea ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Nsekela alikwenda kwa lengo la kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa aliyeambatana na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad