HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 28 November 2018

KITUO CHA UWEZESHAJI SEKTA YA USAFIRI WA KATI WAKUTANA KUJADILI SERA MBALIMBALI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkutano wa Kituo cha Uwezeshaji wa Usafiri wa Kati (CCTTFA), kimekutana na wadau kutoka nchi tofauti katika Ukanda wa Jangwa la Sahara kujadili sera mbalimbali.


Mkutano huo utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia Novemba 28- 30 mwaka huu utazungumzia  mpango wa sera za usafiri wa Afrika eneo la kiuchumi jamii ya ushirikiano wa kamati ya usafiri.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa CCTTFA, Capt Dieudonne Dukundane amesema mkutano huu unalenga kujadili masuala mbalimbali ya Kiuchumi kwa nchi washirika na kuhakikisha mafanikio yanafikiwa.

Amesema, CCTTFA ni kituo kinachokutanisha nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Jamhutri ya Kidemokrasia  Congo, Rwanda na Burundi na kukutana pamoja ni kwa ajili ya kufahamu Tanzania wanafanikiwaje kwenye sekta ya usafiri hususani Reli na barabara na hata sisi pia tunajifunza baadhi ya vitu kutoka kwao.

"Tumekutana katika mkutano huu wa siku tatu lengo letu likiwa ni kujadiliana na masuala mbalimbali pia wao wanakuja  kujifunza Tanzania imefanikiwa kwa namna ipi kwenye sekta ya usafiri hasa kwenye reli na barabara ikiwemo na sisi wenyewe kujifunza baadhi ya vitu kutoka kwao,"amesema Dukundane.

Aidha, ameeleza kuwa kila kanda zinakuwa na kazi maalumu katika kuhakikisha mafanikio yanafikiwa ili wakuze uchumi wa mataifa yao,"tukiangalia kwa upande wa Afrika Mashariki hakuna kulipia visa (Kibali) kwa ajili ya kwenda katika nchi za Uganda, Kenya na zingine kitu kinachochochea kukua kwa uchumi wakati nchi zingine za Afrika hakuna hicho kitu,"

"Tutakutana hapa kwa siku tatu tutajadili masuala muhimu kwenye sekta ya usafiri na ukuaji wa uchumi, hata hivyo ukiangalia kwa nchi za Afrika Mashariki watu wanaigia bila kulipia Visa kitu ambacho kinasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo na ukiangalia nchi zingine za Afrika hakuna,"amesema.

Dukundane amesema, kushirikiana kwenye masuala ya usafiri yamekuwa kichochea kikubwa cha uchumi kukua, kuangalia kipi kinaweza kusababisha mzigo kuchelewa.

Hata hivyo, mkutano huo umewakutanisha wadau hao na watajadiliana ushirikiano uliopo katika nchi hizo kwenye sekta ya usafirishaji na masuala mbalimbali ya kimaendeleo kwenye sekta za biashara.


Katibu Mtendaji wa   Kituo cha Uwezeshaji wa Usafiri wa Kati (CCTTFA),  Capt Dieudonundne Dukane akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mkutano huo utakaofanyika kuanzia Novemba 28- 30 mwaka ukiwa na lengo la  kujadili masuala mbalimbali ya Kiuchumi kwa nchi washirika na kuhakikisha mafanikio yanafikiwa.

Washiriki wa mkutano wa mwaka wa  kituo cha Uwezeshaji wa Usafiri wa Kati (CCTTFA) wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad