HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 16 November 2018

Hatutamvumilia mtumishi atakayekuwa chanzo cha upotevu wa mapato serikalini – Nyongo

Na Rhoda James- Morogoro
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewaeleza wahasibu wa madini nchini kuwa wizara haitamvumilia mtu yeyote ambaye atakuwa chanzo cha upotevu wa ukusanyaji wa mapato ya Serekali. Nyongo ameyasema hayo wakati akifunga Mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali ambayo yaliaanza tarehe 12 hadi 15 Novemba, 2018 katika Chuo cha Mazimbu Campus kilichopo mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Nyongo amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato  serikalini.  Akizungumza katika Kikao hicho Nyongo alisema kuwa Viongozi wote wako tayari kutoa msaada wowote masaa 24 hivyo kama kuna mhasibu ambaye atakuwa na uhitaji kwa masuala ya kikazi asisite kuwasiliana nao waati wowote. 

Aidha, Nyongo alieleza kuwa tasnia ya uhasibu ni ya muhimu sana katika sekta ya madini, hivyo ni vyema kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa katika malengo yake akahakikisha kuwa anafikiria lengo la ndani la Wizara la ukusanyaji wa Bilioni 500 linatimizwa. Pamoja na hayo, Nyongo alitoa pongezi kwa wahasibu wote kwa kufanikisha kufikia lengo la wizara katika ukusanyaji wa mapato ya kiasi cha tsh Bilioni 310 kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 na kuwataka jitihada iliyotumika itumike katika kufanikisha lengo la muhula huu wa fedha.

Aidha, Nyongo amemtaka Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Shukurani Manya kuhakikisha kuwakunakuwa na utekelezaji wa maazimio yote waliyoyafikia katika mkutano huo ili kuweza kuboresha utendaji wao na kuongeza mapato ya wzara kwa mwaka wa fedha 2018/19. Akizungumzia moja ya changamoto walizokuwa wakikutana nazo watumishi wa idara ya uhasibu, Mkurugenzi wa Idara ya Uhasibu Athony Tarimo alisema ni katika uandaaji wa ripoti ambayo kwa kupitia mafunzo hayo imepata utatuzi.

Aidha, amemshukuru Naibu Waziri Stanslaus Nyongo kwa utayari wake wa kukubali kufunga mafunzo hayo na kwamba  anatumaini kwamba wahasibu hao watakuwa mabalozi wazuri hasa katika kufundisha wengine ambao kwa namna moja au nyingine hawakuweza kuhudhuria katika mafunzo hayo.
Mafunzo haya yameshirikisha wahasibu wote wa Wizara ya Madini nchini kote na watumishi wa takwimu kutoka Madini pamoja na watumishi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati kwa waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waiohudhuria mafunzo hayo mara baada ya kufunga mafunzo ya Kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali mkoani Morogoro.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Madini na watendaji kutoka Chuo cha Mazimbu Campus kilichopo mkoani Morogoro.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) wakijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Idara ya uhasibu, Anthony Tarimo (wa pili kushoto) mara baada ya kufika katika chuo cha Mazimbu Campus kilichopo Mkoani Morogoro.
 Mwakilishi wa Chuo cha Mazimbu Campus cha Morogoro, Kundasen Swai akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia).
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Chuo cha Mazimbu Campus Mkoani Morogoro, anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uhasibu, Anthony Tarimo.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akihutubia Wahasibu (hawapo pichani) wakati wakiwa katika mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji Mapato ya Serikali mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uhasibu, Anthony Tarimo akihutubia Wahasibu (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji wa Mapato ya Serikalini mkoani Morogoro.
Wahasibu mbalimbali kutoka Wizara ya Madini pamoja na Wahasibu kutoka Tume ya Madini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) wakati wa Mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad