HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 28, 2018

DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akitoa pongezi kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa kufanikisha uunganishwaji wa Wateja wapya 2881 katika mfumo mpya wa ugawaji maji ambao umekamilika kujengwa kwenye miradi tofauti ya Mamlaka hiyo.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imefanikwia kuunganisha wateja wapya 2881 katika mfumo mpya wa ugawaji maji ambao umekamilika kujengwa kwenye miradi tofauti ya Mamlaka hiyo.

Kazi hiyo iliyoanza Oktoba Mosi mwaka huu imeweza kufanikisha kuunganisha wateja wapya na inaendelea kwa kasi kwenye maeneo tofauti ya Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

Akielezea maunganisho hayo mapya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya amesema kuwa mpaka sasa maunganisho mapya yanaendelea kwa kasi katika maeneo ya Salasala, Kilimahewa na Kinzudi, Kiluvya, Kiluvya madukani, Gogono, Hondoro na Kiamba pamoja na  Bagamoyo- Kiembeni.

Amesema, lengo ni kuunganisha wateja wapya 60,000 (Elfu Sitini) katika eneo la Salasala na wateja 100,000 (laki moja) katika eneo lilipo kati ya Kiluvya na Mbezi.

"Wateja wapya 2881 wameshaunganishwa maeneo yaliyopo, idadi ikiwa 1624 kwa Salasala- Kinzudi, Kiluvya- Mbezi 1111 na Bagamoyo 146 hivyo bado kunwa uwezekano wa wateja wengi zaidi kuendelea kuunganishwa,"amesema.

Amesema Katika kuhakikisha kuwa maji yalioongezeka yanawafikia wananchi wengi zaidi hasa katika maeneo ambayo zamani hayakuwa na mtandao wa mabomba, miradi mikubwa na midogo imetekelezwa ikiwemo uoanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini kukiwa na  ujenzi wa matenki ya maji matano yenye ujazo wa kati ya lita milioni 5.0 na 6.0 pamoja na ulazaji wa mtandao wa mabomba.

Msuya amesema, maeneo hayo yote yanapata maji kutoka katika mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini na ili kuharakisha kazi ya uunganishwaji wa majisafi kwa wananchi wote, wananchi wanakumbushwa kuwa uunganishwaji mpya unatolewa kwa Mkopo.

Aidha, ameeleza kuwa DAWASA itagharamia vifaa, uchimbaji wa mtaro na mabomba ya maji yataunganishwa katika malipo ambayo mteja atarerejesha ndani ya muda wa miezi sita.

Matenki hayo  yamejengwa katika maeneo ya Changanyikeni, Salasala,Wazo, Mabwepande na Bagamoyo na katika maeneo yote ya miinuko ili kuwezesha maji kufika katika maeneo mengi Zaidi kwa msukumo mzuri na mradi huo umetekelezwa na serikali kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya Exim ya India.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad