HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 12 October 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAPONGEZA PRECISION AIR

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewapa sifa Shirika la Ndege Precision Air kwa huduma nzuri wanazotoa kwa wananchi.

Hayo aliyasema baada ya kupita katika banda la shirika hilo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Nchini yanayofanyika kwenye Ukumbi  wa Kimataifa wa JNICC.

Maonesho hayo yamezinduliwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yamehusisha makampuni na watoa huduma za utalii zaidi 300 duniani.

Akizungumza na Michuzi Blog, Meneja Masoko na Mahusiano wa Precisoon Air Hillary Mremi amesema kuwa wamefurahi sana kuweza kupewa pongezi na Waziri Mkuu baada ya kuona juhudi zao katika usafiri wa anga.

Mremi amesema kuwa wamekuwa wanatoa huduma ya usafiri wa anga kwa kipindi cha miaka 25 na wamefanikiwa kupeleka huduma hiyo sehemu tofauti katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda na Kenya.

Mbali na hilo, Mremi amesema kuwa katika banda lao ndani ya maonesho ya kitalii wanatoa huduma ya ukataji tiketi kuelekea sehemu mbalimbali kwa punguzo la bei ikiwemo ofa ya Miliki Anga inayopatikana kwa sh. 150,000 kwa safari za Kilimanjaro, Arusha na Mwanza. Pia wateja wataweza  kuunganishwa na program ya wasafiri wa mara kwa mara ya PAA royal.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika banda la Shirika la Ndege Precision Air na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutoa huduma ya usafiri wa anga  wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Nchini yanayofanyika kwenye Ukumbi  wa Kimataifa wa JNICC.
Meneja Mauzo Kanda ya Pwani Najma Ndasiwa (Kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mteja aliyefika kwenye banda la  Shirika la Ndege Precision Air kwa ajili ya kupata huduma, kushoto ni Meneja wa PAA Royal Hilda Lema wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Nchini yanayofanyika kwenye Ukumbi  wa Kimataifa wa JNICC.
Meneja Masoko na Mahusiano Hillary Mremi akimpa maelezo mteja aliyefika katika banda la Shirika la Ndege Precision Air kwa ajili ya kupata huduma wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Nchini yanayofanyika kwenye Ukumbi  wa Kimataifa wa JNICC.
Wafanyakazi wa  Shirika la Ndege Precision Air wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Nchini yanayofanyika kwenye Ukumbi  wa Kimataifa wa JNICC.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad