HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 2 October 2018

WANAHABARI KUPEWA UBOBEZI WA HABARI ZA NISHATI JADIDIFU

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KATIKA kukuza na kuendeleza sekta ya nishati nchini Kampuni ya Nukta Afrika kwa kushirikiana  Energy Change Lab pamoja na Hivos wameandaa mafunzo rasmi na endelevu kwa  wanahabari ili kuweza kuwajengea uwezo wa kuhabarisha habari za nishati jadidifu  ambayo ni muhimu katika kujenga uchumi wa viwanda na kupunguza gharama za umeme unaotoka katika gridi ya taifa.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa  Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri(TEF)  Deodatus Balile ameeleza kuwa mafunzo hayo kwa wanahabari yatatolewa na wabobezi na mada zitakazotolewa na pamoja na namna ya kufanya tafiti kuhusiana na nishati na kuthibitisha/kutetea  maandiko yao.

Amesema  kunauhitaji mkubwa wa nishati jadidifu  nchini kwani sekta zote hutegemea nishati licha ya tafiti kuonesha kuwa nyumba 3 kati ya 4 hutumia kuni au mkaa na kuna maeneo ambayo yapo nje ya gridi ya taifa kama vile visiwa vya Ukara ambako ni ngumu kupeleka nguzo kwa ajili ya umeme ila matumizi ya sola yanaweza kutatua changamoto hiyo na wananchi kupata huduma stahiki.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Nukta Afrika Nuzulack Dausen amesema kuwa jukwaa hilo lililowahusisha wanahabari ni kwa malengo ya kuwaongezea ufanisi kwa kuwa sekta ya nishati hugusa kila mtu hasa katika sekta za afya na viwanda.

Pia amesema kuwa kupitia mafunzo hayo endelevu wanaamini idadi ya wawekezaji katika sekta hiyo itaongezeka ili kuweza kuokoa maisha ya watu hasa akina mama wanaojifungua katika maeneo ya vijijini.

Kwa upande  Mratibu wa The Energy Change Lab Sisty Basil amesema kuwa jukwaa hilo kwa waandishi litakalotoa mafunzo kwa muda wa miezi 6 ni endelevu na litawajengea  uelewa pindi wanaporipoti habari  kuhusu nishati.

Ameeleza kuwa mahitaji na huduma katika sekta ya nishati kwa sasa ni ya kuridhisha kwani asilimia 90 ya malengo yamefanikiwa katika kuwaunganishia wateja huduma hiyo huku serikali ikiwa na malengo ya kufika asilimia 70 katika sekta ya nishati. 
 Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini (TEF) Deodatus Balile akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya waandishi wa habari kuhusiana na uhabarishaji wa habari za Nishati Jadidifu  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Nukta Afrika  Nuzulack Dausen akizungumza kuhusiana na mtaumizi ya habari za takwimu katika uandishaji habari katika eneo la habari za Nishati Jadidifu , uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa The Energy Change Lab Sisty Basil akizungumza kuhusiana na matumizi ya nishati zilizopo nchini kwa takwimu wakati uzinduzi wa mafunzo ya waandishi wa habari katika eneo la matumizi ya nishati mbadala .
Picha ya pamoja waandaji wa mafunzo pamoja na wahariri wa habari pamoja na waandishi wa habari

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad