HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 5 October 2018

WANACHUO WA KIUT KUENDELEA NA MASOMO OKTOBA 29 MWAKA HUU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Tanzania Kampala(KIU) umewataka wazazi kuondokana na wasiwasi kwani chuo hicho hakijafungiwa wanafunzi waliopo wataendelea na masomo.

Chuo cha Kampala kitaendelea na masomo yake kwa wanafunzi wanaoendelea katika kitivo cha Sayansi na chuo kitafunguliwa Oktoba 08 na kwenye kitivo kingine watafungua Oktoba 29 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mahojiano yake na waandishi wa habari, Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Jamidu Katima amesema kuwa wamekuwa wanapokea simu nyingi sana kutoka kwa wazazi wa wanafunzi wanaosoma kwenye chuo hicho.

Profesa Katima amesema kuwa, chuo chao hakijafungiwa kama walivyosikia katika vyombo mbalimbaki vya habari bali wamesimamishwa kudahili wanafunzi wapya mpaka pale watakapokamilisha baadhi ya changamoto zilizoanishwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

"Ni kweli chuo chetu kimesimamishwa kudahili toka mwaja 2017 na hilo lilikuja baada ya kushindwa kukidhi baadhi ya vigezi vilivyokuwa vimewekwa na tume ya vyuo vikuu na tutakapokuwa tumekamilisha tutaanza kudahili tena," amesema Profesa Katima.

Amesema, taarifa ya tume ya vyo vikuu iliyotolewa hivi karibuni ilivigawa vyuo katika makundi matatu ambayo kundi la kwanza ni vyuo vilivyofungiwa, la pili ni vyuo vilivyoambiwa wahamishe wanafunzi wao na kukatazwa kudahili ili chuo cha Kampala kipo kundi la tatu la kusimamishwa kudahili kwa mwaka huu.

Profesa Katima ameeleza kuwa, kulikua na changamoto mbalimbali katika Chuo chao na kipindi Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako alivyotembelea akiwa na viongozi wa TCU na maafisa uhamiaji aliviona na kuwapatia miezi sita ya kuhakikisha wanayafanyia kazi.

Ameeleza kuwa, moja ya vigezo walivyotakiwa kuvitimiza ni kuwa na walimu wa Shahada ya kwanza  wenye GPA ya 3.5 kwa shahada ya pili  GPA 4.5 na hilo wameshalifanyia kazi kwa kuwaondoa walimu wote ambao hawajakidhi vigezo hivyo pamoja na wale walimu wa kigeni waliokosa vibaki vya kazi na kuishi.

Aidha, katika kukidhi vigezo kama walivyoagizwa na tume ya vyo vikuu Profesa Katima amesema kuwa wamepunguza vitivo kutoka 7 hadi 3 ili kuweza kupata walimu watakaojitosheleza kulingana na maagizo waliyopewa ya kuwa na walimu wanne kwenye kila somo, kupunguza idara kutoka 21 hadi 10 vyote ni katika kuhakikisha wanakamalisha maagizo yote.

Aliongezea kwa kuwataka wazazi watambue kwamba chuo chao bado kinaendelea na masomo ila wapo kwenye jitihada za kukamikilisha yale waliyoambiwa na tume kabla ya muda waliopewa kuisha na mpaka sasa takribani walimu wenye vigezo zaidi ya 60 wameshawaajiri.

Chuo hicho kimesimamishwa kudahili toka mwaka 2017 wakipewa muda wa kufanyia marekebisho changamoti zilizopo chuoni kwao na kupewa masharti ya kunyang'anywa leseni ya kudumu iwapo hawatakidhi vigezo.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Tanzania Kampala(KIU) Profesa Jamidu Katima akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taswira mbalimbali zilizowekwa na wazazi pamoja na wanachuo kuhusu kusimamishwa kudahili wanafunzi wapya mpaka pale watakapokamilisha baadhi ya changamoto zilizoanishwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) leo katika ukumbi wa Chuo hicho.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad