HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 3 October 2018

WANACHAMA NA WAFANYAKAZI NCHINI WATAKIWA KUPITIA UPYA  SHERIA YA MIFUKO YA PENSHENI

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.
Chama cha waajiri nchini ATE wamefanya Mkutano wa pamoja kwa kukutana na wanachama na wafanyakazi  kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa kuungana kwa mifuko ya jamii nchini na kuunda PSSSF.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha waajiri ATE  Dr Aggrey Mlimuka amesema sheria mpya ya waajiri iliyotolewa Agosti Mosi mwaka huu imebainisha taratibu zote za kujiunga na mifuko hiyo.

Amesema kuwa, kwa upande wa waajiri wanatakiwa kuhakikisha waajiriwa wao wanajiunga na mifuko hiyo ya kijamii NSSF,GEPF na Mfuko wa Taifa wa bima ya  afya NHIF ili kupata haki na wajibu .

Kaimu Katibu  wa Mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya jamii SSRA Joseph Mutashubilwa  ameeleza  lengo la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha kila mfanyakazi anajiunga na mifuko hiyo ya NHIF,PSPF,GEPF na kupitia upya sheria iliyoanza kutumika rasmi mwaka huu mwezi Agosti ambayo Ina mamlaka ya kusimamia mifuko ya jamii.

Aidha , Mutashubilwa amesema fursa waliyopata waajiriwa katika elimu hiyo wataweza kusambaza kwa waajiri wao ili kuhakikisha wanapata haki zao bila changamoto yoyote japo kumekuwepo kwa tatizo la waajiri hao kupangiwa sehemu za kupata huduma za kiafya na kulazimika kwenda mbali na maeneo ambayo wanayoishi.

Ametoa fursa kwa wanachama hao kuwasilisha malalamiko yao katika ofisi zao zilizopo Dar es salaam ,Dodoma au kutuma barua pepe.

Katika hafla hiyo  Mwanachama  wa ATE  ambae ni Meneja rasilimali watu kutoka kampuni ya PSSI  Hollyness Mongi ametoa ufafanuzi kwa mifuko hiyo kuungana na kuwa chini ya SSRA.

 Mongi ameshukuru Mkutano  wanachama walikua Kwenye sintofahamu kutokana na Mabadiliko ya utaratibu wa mifuko hiyo kuungana na kupelekea wafanyakazi wapya kutojua taarifa sahihi ya kujiunga na mifuko hiyo upya.
 Mkurugenzi Mtendaji wa chama cha Waajiri nchini ATE Dr. Aggrey Mlimuka akizungumzana na wadau pamoja na waajiri katika hafla fupi ya kutambulisha sheria mpya ya Mifuko ya pensheni jijini Dar es Salaam
Kaimu Katibu wa Mamlaka ya udhibiti wa Mifuko ya pensheni nchini (SSRA) Joseph Mutashubilwa akizungumzana na wadau kuhusu kuungana kwa mifuko ya jamii nchini na kuunda PSSSF.
 Meneja rasilimali watu kutoka kampuni ya PSSI Hollyness Mongi   akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sheria mpya kwa Waajiri pamoja na waajiriwa kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama na wafanyakazi  kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa kuungana kwa mifuko ya jamii nchini na kuunda PSSSF.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad