HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 3 October 2018

PRECISION AIR NA GSM KUWANUFAISHA WATEJA WAO

Meneja Masoko na Mahusiono wa Precision Air Hillary Mremi akizungumzia kuhusiana na mkataba huo walioingia baina ya Shirika la ndege la Precision Air na kampuni ya GSM utakaowaruhusu wateja wa PAA Royal kuoata punguzo la bei la asilimia 15.

Shirika la Ndege la Kitanzania Precision Air, limeendelea kuongeza thamani ya programu yake ya wasafiri wa mara kwa mara ‘PAA ROYAL’ kwa kuongeza faida za unachama wa progamu hiyo na  kusaini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya GSM kuwawezesha wanachama wa PAA ROYAL kujipatia punguzo watembeleapo maduka ya GSM. 

Kupitia ushirikiano huo kati ya Precision Air na GSM, ushirikiano ambao ni wakipekee Tanzania, wanachama wa Paa Royal watajipatia punguzo la hadi asilimia 15 watembeleapo maduka ya Max, Splash and Baby Shop na punguzo la hadi asilimia 10 watembeleapo duka la samani la Danube.  

Akizungumzia ushirikiano huo, Meneja Masoko na Mahusiono wa Precision Air Hillary Mremi amesema, sikuzote wamekua wakionyesha mfano katika kubuni na kutoa huduma za kipekee, ikiwa nijitihada za kuhakikisha wateja wanafurahia safari zao kipekee wasafiripo na Precision Air.

“Kupitia programu yetu ya Paa Royal ambayo ndiyo ya kwanza na pekee Tanzania, wateja wetu wanapata thamani zaidi ya safari wanazofanya nasi. Mteja anaposafiri na Precision Air safari yake haishii tu pale unapofika mwisho wa safari bali anaendelea kufurahia huduma zetu hata baada ya safari katika maisha yake ya kila siku," amesemaMremi

“Tumefurahi kushirikiana na GSM moja ya kampuni zinazoheshimika Tanzania na tunatarajia uhusiano huu utazaa matunda kwa pande zote mbili. Tunawataka wasafiri kuchangamkia fursa ya ushirikiano huu kwa kuchagua kusafiri na Precision Air na Kujiunga na program ya PAA ROYAL ili waweze kufarahia faida za uwanachama.” Amefafanua zaidi Mremi.

Kwa upande wa GSM, Mkurugenzi Mkuu wa Maduka ya GSM Fahad Hamid amesema GSM ikiwa inaongoza katika uuzaji wa bidhaa za mavazi na majumbani, wanafurahi kushrikiana  na shirika linaloheshimika kama Precision Air. 

"Huu ni muendelezo wa mikakati yetu  ya kuhakikisha bidhaa zetu zinapatikana kwa bei nafuu na kuwafikia watu wengi zaidi kupitia ushirikiano na mashrika yanayoheshimika hapa nyumbani.”amesema Hamid.

‘Kupitia ushirikiano huu, Wanachama wa PAA ROYAL watajipatia punguzo maradufu watakapotembelea maduka yetu ya  Max, Splash, Baby Shop na Danube yaliyopo Msasani Mall, Pugu Mall, Mlimani City na  Aura Mall yote yakiwaDar es Salaam. Tunatarajia kuwa na ushirikiano wenye tija na Precision Air na kutoa huduma bora kwa wateja wetu. ‘

Huu unakuwa ni mkataba wa mwingine baada ya Precision Air kusaini na Kampuni ya Max Malipo kwa ajili huduma ya uuzaji wa tiketi kupitia mtandao.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad