HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 15, 2018

WAFANYABIASHARA HAPA NCHINI WAMECHANGAMKIA FURSA YA KWENDA KUSOMA NA KUTAFUTA MASOKO NCHINI CHINA.

Na Agness Francis,blogu ya Jamii.
Katika kuendeleza Tanzania ya viwanda wafanyabiashara wa kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini   wamejitokeza kwa ajili ya kusafiri nchini China kwa lengo kujifunza mbinu za kufanya biashara  pamoja  kutafuta masoko.

Naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki dkt Damas  Ndumbalo amezungumza na wafanyabiashara hao wakati wa mkutano Jijini Dar es Salaam  ambapo aliwapongeza kwa kutaka kuleta maendeleo ya nchi kwa kujituma kutafuta masoko nchi za nje  pamoja na kujifunza namna ya kuanzisha  na  kuendesha viwanda kwa ujumla.

"Njia ya kujikwamua kiuchumi  hapa nchini ni kuwa na viwanda pamoja na kuwekeza nguvu  katika kilimo ambacho malighafi nyingi hupatikana humo,tukasake masoko, teknolojia ya viwanda ambazo zinatumia malighafi zetu za ndani"amesema dkt Ndumbalo.

Aidha mratibu wa safari ya china kushirikiana na BBIC Godwin Msigwa amewapongeza wafanyabiashara na wakulima hao wenye nia ya kutaka kujifunza pamoja na kutafuta masoko nchini humo ambayo ni nchi iliyoendelea kiuchumi hapa duniani.

Mfanyabiashara na mkulima wa mkonge  Hassani Ndimbo kutoka Tanga amezungumza na michuzi blog ambapo amesema ametumia fursa hii ya kujumuika kuelekea nchini china kwa ajili ya kujifunza zaidi mbinu za kufanya bishara na kutafuta masoko.

Vile vile Mmiliki na Mkurugenzi wa shule ya kilimani Mary Kissila kutoka Arusha amesema kuwa anatamani kufanya biashara ya kufuga kuku wa mayai na wanyama,matumaini yake ni  kupata  mafunzo na mbinu ambazo zitamuwesha  kufanya biashara hiyo katika  safari yake ya kwenda nchini china.

"Nawasii wakina mama wenzangu wasikate tamaa fursa kama hizi zipo wajitokeze kuzitumia kwa ajili ya maendeleo yao na kwa jamii nzima"amesema Mary.
 Naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Damas Ndumbalo akiwa anazungumza na wafanyabiashara na wakulima kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini wanaosafiri kuelekea nchini China kujifunza mbinu za kufanya biashara pamoja na kutafuta masoko,Jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka kutokukata tamaa na waongeze nguvu katika kuleta naendeleo katika kuelekea Tanzania ya viwanda.
 Meneja Mkuu kampuni ya BBIC Zhu Huojian  akitoa mafunzo kwa wafanyabiasha na wakulima hao kuhusu mbinu za kufanya biashara  na kukuza viwanda,Jijini Dar es Salaam.
 Naibu waziri wizara ya mambo ya nje na ushirukiano wa Afrika Mashariki Damas Ndumbalo,akizungumza Jijini Dar es Salaam  na wafanyabiashara wanaosafiri kuelekea nchini China kujifunza namna jinsi uendeshwaji wa biashara unavyokuwa nchini humo pamoja na kutafuta masoko.
Naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje na uhusiano wa Afrika Mashariki Damas Ndumbalo akiwa katika picha ya pamoja Jijini Dar es Salaam  na wafanyabiashara wanaosafiri kuelekea nchini China kwa ajili ya mafunzo zaidi ya kibaishara na kutafuta masoko ili kukuza uchumi wa nchi yetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad