HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 8 October 2018

“VITENDO VYA UKEKETAJI KWA WATOTO WADOGO NCHINI VICHUNGUZWE”- DKT. NDUGULILE.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari kutoka  vyombo mbalimbali vya habari wakati wa mdahalo wa wahariri wa vyombo vya habari nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuhusu namna bora ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa mtoto wa Kike kuelekea Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike 2018.
 Katibu Mkuu Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto John Jingu akielezea jitihada za Wizara katika kukabiliana na vitendo vya uaktili kwa watoto wa kike kwa vyombo vya habari wakati wa mdahalo wa wahariri wa vyombo vya habari nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuhusu namna bora ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa mtoto wa Kike kuelekea Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike 2018.
 Baadhi ya Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari na wadau wa mtoto wa kike wakifuatilia mdahalo wa Kitaifa kuliofanyika jijini Dar es Salaam   kuhusu namna bora ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa mtoto wa Kike kuelekea Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike 2018.
Katibu Mkuu Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto John Jingu akiwa katika picha na viongozi nz wajumbe wa Baraza la watoto la taifa na wadau wa maendeleo na ustwi wa Mtoto mara baada ya kumalizika kwa mafunzo kwa watoto kuhusu mimba na ndoa za utotoni yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Kitengo cha Mawasilianio WAMJW

Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam.
Serikali imeagiza kuchunguzwa kwa vitendo vya ukatili hasa ukeketaji kwa watoto wachanga unaondelea kufanyika nchini kwa baadhi ya makabila yenye mila za ukeketaji wamebadili mbinu na kuanza kukeketa watoto wachanga kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo wakati akiongea na vyombo vya habari katika mdahalo wa wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana masuala ya ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni.

Naibu Waziri Ndugulile amesema kufuatia jamii hizo kubadili mwenendo wa ukeketaji na Serikali kubaini mbinu hizo amesisitiza agizo lake alilolitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika Mkoani Arusha la kuwataka madaktari wote nchini kufanya uchunguzi kwa watoto wote wachanga ili kubaini kama watoto hao wamefanyiwa ukatili kwa kukeketwa ili wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Dkt. Ndugulile aliongeza kuwa utafiti unaonesha kuwa takwimu za mimba za utotoni bado ziko juu Nchini nakutaja mikoa inayoongoza kwa mimba za utotoni kuwa ni Katavi 45%, Tabora%, Morogoro 39%,Dodoma 39%, na Shinyanga 34%.

Aidha ameamuagiza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kushirikiana na Idara Kuu ya Afya kuona namna bora ya kupamba na vitendo hivyo na kuhakikisha vitendo vya ukeketaji kwa watoto wachanga vinakomeshwa nchini.

Pia Dkt. Ndugulile ameviambia vyombo vya habari kuwa takribani asilimia  37 ya wasichana nchini wanaolewa kabla ya miaka 18 na kutaka jamii kuwapeleka wasichana shuleni kwani kadri msichana anavyokaa shuleni ndivyo anapunguza uwezekano wa kupata watoto na kuolewa mapema lakini pia elimu inamuwezesha kupata pato la uhakika.

‘’Msichana anavyozidi kukaa shuleni ndivyo anavyopunguza hatari ya kupata mimba ya utotoni na kadili anavyozidi kukaa shuleni ndivyo anavyoepukana na ndoa za utotoni lakini pia elimu inamwezesha msichana kuwa na kipato cha uhakika kuendesha maisha yake”. alisema Dkt. Ndugulile.

 Wakati huo huo Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. John Jingu amesema kuwa watoto ni ndio hazina ya Taifa nakutoa wito kwa jamii nchini kuwekeza vyema katika watoto ili hapo baadae nchi iweze kuwa na maendeleo endelevu.

Aidha Dkt. John Jingu amesema maadhimisho ya mwaka huu ni fursa kwa jamii kuendeleza mapambano ya vitendo vyote vya ukatili dhidi ya mtoto wa kike ikiwemo changamoto zinazowakabili watoto hao hasa kwa baadhi ya jamii ambazo bado zinaendelea na vitendo vya ukeketaji na ndoa za utotoni.

 Amewataka waandishi wa habari kutoa kipaumbele katika uandishi wa masuala ya watoto kwa kuzingatia kuwa watoto ndio ustawi wa jamii ijayo ya watanzania kwa kuwa kuzungumzia watoto maana yake unazungumzia Taifa la kesho.

Mdahalo huo unafanyika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike kwa mwaka 2018 kufanyika Mkoani Dar es Salaam na kilele cha maadhimisho hayo ufanyika kila mwaka tarehe 11 mwezi wa kumi kufuatia agizo la Umoja wa Mataifa la mwezi Desemba mwaka 2011 ni kuzitaka Nchi Wanachama wa Umoja huo kuadhimisha siku hii ili kuwalinda watoto wa kike dhidi ya ukatili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad