HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 25 October 2018

UNESCO kufunza elimu ya dijiti kwa wanafunzi 200


 Mkufunzi Kiongozi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Bw. Wilhelm Oddo akitambulisha msafara aliombatana nao akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Nancy Kaizilege(wa tano kushoto) kwenye ofisi za walimu wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwa ajili ya mafunzo ya Tehama kwa wasichana wa shule hiyo wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Nancy Kaizilege akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chanzige iliyopo wilayani Kisarawe kuhusu nafasi ya vijana katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoambatana na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo  hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
 Mkufunzi Kiongozi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Bw. Wilhelm Oddo akitoa utangulizi wa elimu ya Tehama kwa baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe. Haya ni moja kati ya mafunzo ya Tehama yameandaliwa na Shirika hilo lisilo la kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO  wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yenye lengo la kuongeza ushiriki wa mtoto wa kike katika masomo ya Sayansi, Tehama, Uhandisi na Mahesabu (STEM) yaliyoambatana na sherehe za  maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo  hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
 Wakufunzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Balbina Gulam (kushoto) na Raymond Benedict (kulia) wakiendesha mafunzo ya Tehama kwa vitendo kwa baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.

 Baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe wakishiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
 Mkufunzi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Balbina Gulam ambaye pia ni mwanzilishi wa tovuti ya Hudumasmart akitoa maelekezo kwa wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe kwenye mafunzo ya Tehama kwa vitendo yaliyoendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
 Afisa kutoka kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Justin Mori akifafanua jambo kwa baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo yalioandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
 Baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.

 Baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo wakizungumzia muktadha wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu-SDGS na changamoto zinazowazunguka kwenye maeneo wanayoishi wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
 Mwanzilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima akizungumza na baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo yaliyoandaliwa na Shirika hilo lisilo la kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.


 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Nancy Kaizilege (kulia) na Mwanzilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima (kushoto) wakikabidhi vyeti kwa baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo yaliyoandaliwa na Shirika la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
  Baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo yaliyoandaliwa na Shirika la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Nancy Kaizilege na Mwanzilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo yaliyoandaliwa na Shirika la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limepanga kufunza wanafunzi 200 kutoka shule sita nchini namna ya kutengeneza mfumo wa alama zinazotumiwa katika maandishi ya kompyuta na matumizi yake.
Wanafunzi hao 200 watakuwa miongoni mwa vijana zaidi ya 2,489 waliofunzwa kuendeleza utaalamu wa kidijiti kwa ajili ya maendeleo.
Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO, katika kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa yenye kauli mbiu “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” mafunzo yalifanyika katika shule ya sekondari ya Chazinge.
Hatua hizo zimelenga kuwezesha njia ya kuelekea uchumi wa viwanda nchini Tanzania.
Pamoja na shule ya sekondari ya Chazinge na Kimani iliyopo Kisarawe mkoani Pwani nyingine ni Jamhuri, Gerezani na Benjamin Mkapa zilizopo Ilala mkoani Dar es Salaam.
Katika mafunzo hayo UNESCO watahakikisha kwamba vijana wanakuwa wavumbuzi, wabunifu na hivyo kutumiwa kuboresha namna bora ya kufanya biashara miongoni mwa vijana wa kike na wakiume.
Taarifa hiyo imesema kwamba lengo kuu ni kuwezesha vijana hasa wanawake kutumia kikamilifu mifumo ya tehama kujiendeleza katika masomo ya  Sayansi, Tehama, Uhandisi na Mahesabu (STEM).
Alisema mafunzo hayo yataongeza pia uwezo wa vijana kujiajiri na kuajiriwa kwa kuwa na ujuzi zaidi.
Mradi wa mafunzo hayo ni sehemu ya mradi wa UNESCO unaofanyiwa kazi katika nchi zaidi ya 25 unatambuliwa kama Youth Mobile Initiative kwa lengo la kuboresha hali za uchumi za mataifa hayo kupitia matumizi ya kompyuta.
UNESCO katika kuendeleza vijana imeshirikiana na Apps and Girls kuendesha tamasha la nne la Africa Code Week linalofanyika katika nchi 36 za Afrika tangu lianzishwe mwaka 2015.
Imeelezwa katika taarifa hiyo kwamba jumla ya vijana milioni 1.8 wamefunzwa masuala ya dijiti kuelekea karne ya 21.
Mafunzo hayo yamalenga kuhakikisha kwamba wanakuza uwezo wao wa kutumia alama za siri kutengeneza programu mbalimbali kwa matumizi anuai.
Wakizungumza siku hiyo katika muktadha wa SDGS wanafunzi wa shule ya sekondari Chazinge walitaka wataalamu kuhakikisha kwamba malengo hayo yanatekelezwa kwa kuweka mazingira rafiki.
Maizngira rafiki hayo ni ya kusoma, makazi katika jamii nakadhalika.
Mwanafunzi Naomi Ashery alisema kwamba mji kama wa Kisarawe hauendelei kutokana na mazingira yake kutokuwa rafiki kwa wawekezaji. Alisema mji huo hauna barabara nzuri, huduma ya umeme na maji ya kuridhisha hivyow atu wanapotaka kujenga japo wamezaliwa Kisrarwe huenda jijini Dar es salaam.
Naye Catherine Francis alisema mazingira ya usalama pia yanatia hofu kutokana na kuwapo wka matukio mengi ya kihalifui hivyo kutotekelezwa kwa malengo endelevu kunachochewa kukosekana kwa usalama.
Grace Rodgers amesema kwamba ipo haja ya wananchi kuanza kutambua umuhimu wa kushirikiana na kuacha ubinafsi ambao ndio msingi mkuu wa uchumi kudidimia katika nyanda hizo.
Anasema mimba za utotoni zinatokana na mazingira kutokuwa safi kwani wengi wanaishi mbali  na maeneo na hivyo wanakuwa katika hatari ya kurubuniwa kirahisi.
Hadija Lugoma alisema kwamba hakuna usawa wa kijinsia kutokana na  watu kutopatiwa elimu hiyo muhimu ili waweze kujitambua.
Eliya Mangi alisema kutokana na kaya nyingi kuwa maskini umaskini hauwezi kumalizwa kutokana na  kushindwa kupata elimu wanayostahili ya msingi na sekondari ambayo itawafumbua macho.
Agnes Philemon alizungumzia lengo la 17 ambapo anasema ukosefu wa ushirikiano umesababisha kukosekana kwa nia njema za kusukuma maendeleo. Alisema watu wengi wametawaliwa na ubinafsi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad