HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 8 October 2018

TANZIA: Msiba Ujerumani wa KONDO MOHAMED MSUMI aka Mguu Mtupu

Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU e.V) kwa masikitiko makubwa tunawataarifu kifo cha Mtanzania mwenzetu   Kondo mohamed Msumi  ambaye alikuwa akiishi  Bochum,nchini ujerumani.
Marehemu Kondo Mohamed Msumi amefariki usiku wa 2.kuamikia 3 Oktoba 2018 akiwa hospitalini akipatiwa matibabu,  kamati ya Umoja  wa Watanzania Ujerumani UTU e.V imewasiliana na ndugu wa marehemu waliopo Ujerumani na Tanzania  Tumeazimia kupitisha michango  ili  kutuwezesha kufanikisha  mazishi ya ndugu yetu, bado hatujajua kwamba tutazika hapa Ujerumani au tutasafirisha, tutawaletea taarifa zaidi kadiri tunavyozipata.
Kamati imechagua Rafiki  wa karibu na familia ya Kondo ili kupokea michango hiyo. Michango yote ipitishwe kwenye acc ifuatayo.

Gls Bank,
Jafari Juma Mazangwi. 
IBAN:DE15 4306 0967 4046 5996 00.
Bic: GENODEM1GLS
Tunawaomba watanzania wote  kutoa michango kwa wingi ili kumuhifadhi ndugu yetu marehemu Kondo Mohamed Msumi
Asanteni

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad