HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 16 October 2018

TAMUFA YAWAPA FURSA WANAMUZIKI 196 KUPATA KADI ZA BIMA YA AFYA NA NSSF

 Naibu Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto Dr.Faustine Ndugulile akizungumzana na Wanamuziki pamoja na wadau  wakati akitoa kadi za bima ya afya.

Na Khadija Seif,Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii,jinsia,Wazee na Watoto ambae pia ni Mbunge wa Kigamboni kupitia chama cha Mapinduzi, Dkt. Faustine Ndugulile  ameshiriki katika zoezi la kugawa pamoja na kujiandikisha kwenye bima ya afya kupitia shirika la (NSSF) kwa Wanamuziki wa bongofleva, kwaya na muziki wa zamani jijini Dar es salaam.

Aidha, Ndugulile amepongeza jitihada zilizofanywa na chama cha Wanamuziki nchini (TAMUFA) kuona fursa hii kusaidia Wanamuziki ili kujijengea akiba ya badae,kupata bima ya afya,mafao ya uzazi na fursa nyingne nyingi.

Kwani Wanamuziki ni sehemu ya ongezeko la pato la Taifa kutokana na wengi wao kufanya shughuli kama sehemu ya biashara.
 Naibu Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii,jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza kwenye hafla hiyo.

Afisa Mkuu Mwandamizi kitengo cha sekta isiyo rasmi (NSSF), Abas Cothema amepongeza chama cha Wanamuziki nchini ( TAMUFA) kwa kuungana nao kuchukua bima za afya kupitia shirika hilo. Cothema ameeleza muitikio wa Wasanii umekua mzuri hivyo basi elimu iliyotolewa imeweza kufika kwa wakati sahihi na mpaka sasa takribani Wanamuziki 196 wameshajiandikisha na bima hiyo. Ameeleza kuwa afya ni muhimili mkubwa sana unaohitajika kuboreshwa kwani afya bora ndio inayomuwezesha mtu kufanya shughuli zake pasipo na kikwazo chochote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanamuziki nchini (TAMUFA) Donald Kisanga ametoa shukrani kwa muitikio huo katika harakati za ukombozi wa Sanaa ya muziki nchini. Kisanga amefafanua dhima kuu ya kuandaa bima za afya kwa Wanamuziki kutokana na Wanamuziki wengi walipoteza maisha kutokana na kutoweza kumudu gharama za vipimo na Matibabu , hivyo wakaweza kujikita  na kuhakikisha wanapatiwa kadi za bima ya afya ili kumudu gharama na  kuondokana na adha hiyo.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya TAMUFA, Donald Kisanga akizungumzana na wanahabari pamoja na wanahabari Katika hafla ya ugawaji wa kadi za bima ya afya jijini Dar es salaam.

Na ametoa shukrani kwa serikali iliyopo Madarakani chini ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ambae wakati anaingia Madarakani alisema serikali ipo tayari kuwasaidia hivyo watunge nyimbo zenye kuunganisha Taifa pamoja na kuimarisha amani.

Kisanga ameomba serikali iweze kuangalia umri wa Mwanamuziki katika suala la matibabu ili waendelee kupata bima ya afya hata wakiwa wazee kwani kazi ya muziki Haina kustaafu, na kwa upande wa msamaha kwa wazee uendelee kuwepo kama wanavofanyiwa kwa upande wa watumishi wengine walio serikalini.

Aidha  Cothema amesema NSSF ina gusa katika nyanja zote na masharti yake ni ya kawaida na ambayo yanamuwezesha hata mtu mwenye kipato cha chini kujiunga, na ametoa wito kwa wasanii wa filamu nchini kujiunga na bima ili kuweza kupata matibabu kwa haraka zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad