HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 10 October 2018

TAMASHA LA URITHI FESTIVAL LAMEZINDULIWA RASMI MKOANI ARUSHA

Ngoma ya Kabila la wamaasai wakiimba katika Tamasha la Urithi Festival lililozinduliwa  Jijini Arusha Katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid .Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya washiriki wakila ugali wa asili na mlenda katika tamasha la urithi festival katika uwanja wa shekh Amri Abeid Jijini Arusha na Vero Ignatus.

Katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Arusha katika Tamasha la Urithi Festival lililozinduliwa mkoani Arusha. Picha na Vero Ignatus
Katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi akiwa katika moja ya banda wanalotengeneza vitu vya asili. Picha na Vero Ignatus. 
Kutoka katikati ni Katibu mkuu wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi, kulia kwake ni Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya Taif a Profesa Audix Mabula ambaye pia ni Mwenyekiti wa maandalizi ya Tamasha la Urithi, akifuatiwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega. Picha na Vero Ignatus.
 Kushoto ni Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audix Mabula, Katibu Mkuu wizara ya habari michezo michezo na Utamaduni Suzan Mlawi wakiwa katika moja ya banda uwanjani hapo. Picha na Vero Ignatus.
Ngoma ya asili ya Wakina mama kutoka kabila la Kimeru. Picha na Vero Ignatus
Hawa nao wakinamama kutoka kabila la Kimaasai walipamba Tamasha hilo la Urithi na utamaduni mkoani Arusha katika uwanja wa Shekh Amri Abeid. Picha na Vero Ignatus.

Na Vero Ignatus ,Arusha
Kila mwaka mkoa unatakiwa kutenga fungu kwaajili ya kuandaa tamasha la urithi na utamaduni itakayochangia  kuzaa zao jipya la utalii na kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi katika uzinduzi wa Tamasha la Urithi lililozinduliwa Jijini Arusha katika uwanja wa Shekh Amri Abeid na kushirikisha makabila mbalimbali mkoani hapo.
Ameeleza  kuwa  Taifa lisilo na utamaduni ni taifa lililokufa, sambamba na kupoteza rasilimaliza  husika kwani utamaduni ni kuvutio kibwa cha utalii.
"Tusipoenzi na kuzitunza tamaduni hizo utu wetu rasilimali zetu zitapotea, kwani utamaduni wetu ni kivutio kikubwa cha utalii"alisema Katibu Suzan


Kwa upande wake Katibu tawala wa
Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema asilima 80%wageni wanaoingia nchini  wanatembelea Mkoani hapo kutokana na vivutio vilivyopo mkoani Arusha kupitia  vya utalii Maonyesho hayo  yamehusisha wadau kuonyesha mambo burudani,ngoma za asili,vyakula vya asili,mavazi ya asili ,utalii na tamaduni za Mtanzania bila kuvunja sheria .
Tutapata nafasi nzuri za kuona tamaduni mbalimbali za kuona mambo mbalimbali, mavazi, vyakula, michezo ya asili.alisema Kwitega.


Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya Taif a Profesa Audix Mabula ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kubuni wazo hilo zuri, kwa kutambua na kuthani, kutafiti na kuhifadhi vitu vya asili kwa manufaa ya Watanzania na kwa vizazi vijavyo.

Ikumbukwe kuwa septemba 15 Tamasha la Urithi Festival lilizinduliwa rasmi Jijini Dodoma na Makamu wa Rais Samia Suluhu likiwa na kauli mbiu isemayo "Urithi wetu Fahari yetu"Maonyesho hayo yamehusisha wadau mbalimbali kuonyesha mambo burudani,ngoma za asili,vyakula vya asili,mavazazi ya asili ,utalii na tamaduni Kuhifadhi tamaduni zetu nzuri


Tamasha hilo la urithi litafungwa tarehe 13 octoba na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uwanjawa Shekh Amri Abeid Arusha.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad