HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 18 October 2018

SERIKALI YAWATAKA WAKUU WA IDARA ZA UTAWALA NA RASILIMALIWATU SERIKALINI KUSIMAMIA VIZURI RASILIMALIWATU

 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akiendesha kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kinachofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akifungua rasmi  kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainab  Chaula akizungumza na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kuhusu masuala ya kiutumishi katika kikao kazi kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko akizungumza na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu waliohudhuria kikao kazi kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

 Baadhi ya Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu serikalini wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha watendaji hao  kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

Serikali imewataka Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Taasisi za Umma nchini kuhakikisha rasilimaliwatu inasimamiwa vizuri ili kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
Dkt.Ndumbaro amesema kuwa, rasilimaliwatu ikisimamiwa vibaya matokeo yake ni kushuka kwa utendaji kazi, na utendaji kazi ukishuka unasababisha uchumi  wa nchi kutokukua inavyotakiwa, hivyo Taifa kushindwa kufikia lengo lake la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Dkt.Ndumbaro amewasisitiza Wakurugenzi wanaosimamia rasilimaliwatu katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala na Mashirika ya Umma kuwa taasisi zote za Umma zifanye kazi kwa pamoja ili kutekeleza vipaumbele vya Taifa.
Aidha, Dkt.Ndumbaro amewakumbusha Wakuu hao wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kuzingatia maadili katika utendaji kazi ili wawe mfano wa kuigwa na watumishi wengine.
Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko amewaasa watendaji hao kuwa washauri wazuri, walezi bora, walimu wazuri  na watatuzi wa changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wanaowasimamia ili wawe na tija katika maendeleo ya Taifa.
Bi. Mwaluko amewataka Watendaji hao kuhakikisha wanasimamia vema nidhamu ya watumishi wa umma ili kujenga taswira nzuri ya utumishi wa umma.
Mkutano kazi huo wa Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma una lengo la kuwakumbusha na kuwahimiza watendaji hao utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kiutendaji, uendeshaji na usimamizi wa rasilimaliwatu kwa kuzingatia malengo,shabaha na vipaumbele vya kitaifa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad