HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 2, 2018

Rais Magufuli atekeleza ahadi ya kutoka Milioni 20 kwa wavuvi na Mama Janeth Magufuli Milioni 5 za mama ntilie eneo la feri jijini Dar es salaam

 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike  akimsikiliza kiongozi wa Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga akishukuru baaada ya kupokea shilingi milioni 5 kutoka kwa mke wa Rais Mama Janeth Magufuli alizoahidi kuwasaidia Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo hilo.
 Wajasiriamali wakishangilia kwa furaha utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) na ya Mama Janeth Magufuli ya kutoa msaada wa shilingi milioni 5 kwa kia na mama waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsikiliza Bw. Amiri Amani, Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam akishukuru kwa msaada wa shilingi Milioni 20 kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli alizowaahidi kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja huo. 
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi  msaada wa shilingi Milioni 20 kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli alizowaahidi kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Umoja huo Bw. Amiri Amani, Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam. 
  Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi msaada wa shilingi milioni 5 kutoka kwa mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa kiongozi wa Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga alizoahidi kuwasaidia Mama wajasiriamali wanaofanya biashara ndogondogo hasa ya Mamalishe katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam. 
 Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwaangalia Makamu Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani na kiongozi wa akina Mama wajasiariamali Bi. Ashura Seif Nanjonga wakiweka sahihi katika hati za makabidhiano ya fedha taslimu kutoka kwa Rais Dkt. Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli huku wakishuhudiwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sofia Mjema, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Tulusubisya Kamalama na mshauri wa Rais Masuala ya sheria Bw. Dunstan Kiobya (kushoto)
Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akiwa na  Mwenyekiti wa UWAWAKI Bw. Amir Amani   wakielekea sehemu itapojengwa ofisi zao katika utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutoa shilingi milioni 20 kwa ajili ujenzi wa ofisi ya Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWAKI) waliopo katika eneo la Feri, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad