HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 2, 2018

NAIBU WAZIRI HASUNGA AHAMASISHA UTALII WA NDANI MASHULENI

NA LUSUNGU HELELA- SONGWE
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga  ameanza ziara ya  kimkakati ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wanafunzi wa  shule za sekondari nchini lengo likiwa ni  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao kwa wanafunzi hao. 
Mhe. Hasunga amesema sekta ya utalii inaweza kuongeza pato lake maradufu iwapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  wataanza kujua umuhimu juu ya utalii wa ndani bado angali wakiwa wadogo.
Katika ziara hiyo aliyoianza mkoani Songwe wilayani Mbozi, Naibu Waziri Mhe. Hasunga ameweza kutembelea shule za Sekondari tatu ikiwemo Shule ya Kilimampimbi, Vwawa pamoja na  Ilolo ambapo amezungumza na wanafunzi pamoja na walimu   kuhusu umuhimu wa utalii wa ndani.
Amefafanua kuwa Wanafunzi ni mabalozi wakubwa wa mabadiliko, wanapopata elimu juu ya  utalii wa ndani wataweza kuifikisha kwa wazazi, walezi pamoja na jamii kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Mhe. Hasunga  ametoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliokuwa wakijibu maswali kuhusiana na vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Amesema sekta ya utalii inachangia  asilimia 17.5 ya pato la taifa na inaweza ikawa asilimia 30 kama kutajengeka utamaduni kwa jamii  wakiwa bado  wanafunzi   kuhusu umuhimu wa kutenga muda pamoja na pesa kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
‘’Nchi yetu imejaliwa kuwa na vivutio vingi lakini imekuwa haifanyi vizuri ukilinganisha na nchi kama Misri aambao wao hawana vivutio vingi kama tulivyonavyo sisi, Wenzetu wana magofu pekee lakini wametuacha mbali’’ amesema Mhe. Hasunga.
Katika kuzungumza na wanafunzi kwa nyakati tofauti, Naibu Waziri Mhe. Hasunga amesema shabaha ya kutoa uelewa huo ni kutaka sekta ya utalii iiongeze mapato yatakayosaidia katika kuleta maendeleo nchini. 
Katika hatua nyingine, Mhe. Hasunga amesema utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii kwa wanafunzi ukishajengeka kutasaidia kuleta mapinduzi ya sekta ya  utalii na kuaachana na hali ya  kutegemea watalii kutoka nje ambao wakati mwingine hupungua na kusababisha mtikisiko wa kimapato.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Kilimampimbi,  Joshua Ng’onda     amesema kwa kutambua mchango mkubwa wa sekta ya utalii katika pato la Taifa, utalii wa ndani unapaswa kuchochewa tangu darasani. Ni wajibu wa kila shule kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafundishwa umuhimu wa kutalii mara nyingiza zaidi kwaajili ya kujenga utamaduni.

Naye Mwanafunzi wa Vwawa, Anna Njawike amesema kitendo cha Naibu Waziri kuwatembelea katika shule yao ni faraja kubwa na amefungua ukurasa mpya kwa wanafunzi walio wengi kujenga tabia ya kutumia likizo kwenda kutalii.
Ameongeza kuwa ni rahisi kwa wanafunzi kujengewa utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii wakiwa bado  wadogo na kuachana na imani iliyojengeka kuwa   vivutio vya utalii vipo tu kwa ajili ya wageni pekee.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kilimampimbi iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini  kwa lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao. 
 Baadhi ya wanafunzi wa Vwawa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Vwawa iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa  lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (katikati)  akizungumza na walimu wa  shule ya sekondari ya Vwawa  iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe mara baada ya kumaliza   kuzungumza na  wanafunzi wa shuke hiyo  kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilolo  iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe  akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa  lengo la  kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbozi, Bi. Hossana Mshule wakati w akielekea kukagua baadhi ya majengo yaliyojengwa kwa mfuko wa jimbo la Vwawa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga   akiwa ameongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ujenzi  wa jengo  lilijengwa kwa ajili ya wnafunzi wa shule Vwawa akiwa na kamati ya Ujenzi wa jengo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad