HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 12 October 2018

Mkoa wa Kagera wavutiwa na uwekezaji wa TADB

Na mwandishi wetu
Serikali ya mkoa wa Kagera imepongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) kwa kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 31 katika sekta ya kilimo mkoani kagera hali inayoongeza tija ya uzalishaji katika kilimo mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine aliyekuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya kilimo inayopatiwa mkopo na benki hiyo.

Brigedia Jenerali Gaguti amesema kuwa uwepo wa Benki ya Kilimo katika tasnia ya kahawa mkoani kagera imeweza kusaidia ulipaji wa malipo ya awali ya shilingi 1,000 kwa kilo moja ya kahawa ya maganda kwa mkulima mdogo mkoani humo.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema Benki ya Kilimo inaendelea kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara na kwa sasa benki inalenga katika kuhamasisha unywaji wa kahawa ili kuongeza soko la ndani kwa zao la kahawa.

Bw. Justine ameongeza katika kuchagiza uwekezaji katika sekta ya kilimo mkoani humo, TADB imejipanga kuongeza idadi ya mazao ya kilimo yatakayopewa kipaumbele katika mikopo inayotolewa na benki hiyo hasa kwa miradi ya kilimo cha umwagiliaji.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti (kulia) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake mkoani Kagera.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine na ugeni wake (hawapo pichani) mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake mkoani Kagera. Ugeni huo ulikuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya kilimo inayopatiwa mkopo na benki hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza wakati yeye na timu yake walipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti (hayupo pichani) na kuzungumza nae kuhusu masuala ya uwekezaji katika mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika kilimo. Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Tathmini na Ufuatiliaji wa TADB, Bw. Stephen Kang'ombe.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akizungumza wakati yeye na timu yake walipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti (hayupo pichani).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad