HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 14, 2018

Mhini, Sonia waonyesha cheche zao katika Olimpiki ya Vijana, Argentina

Na Mwandishi wetu
Muogeleaji anayekuja kwa kasi katika mchezo huo hapa nchini, Dennis Mhini amevunja rekodi ya muda wake katika michezo ya vijana ya Olimpiki inayoendelea Buenos, Argentina katika staili ya backstroke ya mita 50 na freestyle ya mita 100.

Mhini ambaye ameshiriki katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza alimaliza katika nafasi ya tatu kwa upande wa mita 100 freestyle kwa kutumia  sekunde 58.53 na kujizolea pointi 514 wakati kwa upande wa mita 50 backstroke, alitumia muda wa sekunde 29.79 na kupata pointir 525 baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu.

Muogeleaji huyo amoenyesha kuwa ni lulu ya nchi katika mashindano yajayo ya kimataifa ikiwa ya Jumuiya ya Madola, Olimpiki ya wakubwa na mashindano ya dunia ya kuogelea.

Mbali ya Mhini, pia muogeleaji wa kike, Sonia Tumiotto naye aliweza kufanya vizuri pamoja na wote wawili kushindwa kuingia fainali.

“Waogeleaji wetu bado wadogo sana na wamekutana na changamoto nyingi za kiufundi. Makocha wao wamejitahidi sana kuwafikisha katika hatua ya juu, lakini hakuna vifaa vya kisasa kulinganisha na nchi nyingine,”

“Hatuna maswawa ya kisasa ya kuogelea, hali imewafanya waogeleaji kuwahi kuondoka kuelekea kwenye mashindano kwa lengola kufanya mazoezi kwenye mabwawa hayo, sisi ni tofauti sana na wenzetu,” alisema kocha Michael Livingstone.

Livingstone ambaye ameongozana na waogeleaji hao, amesema kuwa Mhini na Sonia wamejitahidi sana na alama walizopata ni ishara tosha kuwa mchezo huo unapata mafanikio.

Kwa upande wa Sonia, muogeleaji huyo aliweza kulinda muda wake katika mita 100 na 200 katika mtindo wa freestyle.

Sonia alimaliza kwa kwanza katika kundi la kwanza (heat 1) kwa upande wa mita 100 kwa kutumia muda wa 1.01.47 na kupata pointi 595 na kushika nafasi ya tatu kwa kutimia muda wa 2.12.05 na kupata pointi  626.

Mwenyekiti wa chama cha kuogelea nchini (TSA), Imani Dominick aliwapongeza waogeleaji hao kwa kuhimarisha muda wao pamoja na kutotwaa medali.

“Najua wadau wengi wa michezo wanataka kuona medali, ni kweli, lakini kwa hali ya mchezo wetu ambao ndiyo kwanza unakua, tunaangalia zaidi kuhimarisha muda na kupata muda wa kufuzu, mpaka sasa hatuna hata bwawa la kuogelea la kisasa, bado tunatafuta bwawa pia,” alisema Dominick.
 Dennis Mhini ‘akichapa maji’ katika mchezo wa kuogelea katika michezo ya vijana ya Olimpiki inayoendelea Buenos, Argentina katika staili ya backstroke ya mita 50 na freestyle ya mita 100
 Sonia akionyesha ufundi wake katika kuogelea katika michezo ya vijana ya Olimpiki inayoendelea Buenos, Argentina.
 Dennis akionyesha umahiri wake katika staili ya backstroke
Mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea (TSA) Imani Dominick akisisitiza jambo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad