HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 14, 2018

CCM YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUTELEZA ILANI

Na Tiganya Vincent
HALMASHAURI kuu ya CCM Mkoa wa Tabora imeipongeza Serikali ya Awamu ya tano kutokana na kutekeleza kwa vitendo Ilani yake ya miaka mitano tangu ulipofanyika uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2015 hadi sasa.

Pongezi hizo zimetolewa jana kwenye kikao maalumu cha wajumbe wa Halmashauri hiyo iliyokutana kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kutoka serikali ya Mkoa wa Tabora.

Wajumbe hao walisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dokta John Pombe Magufuli iliahidi miradi mbalimbali kwa wakazi wa Mkoa huo ikiwemo ya maji, afya, barabara na kilimo ambapo utekelezaji wake unaonekana kwa macho.

Waliitaja miradi ambayo utekelezaji wake umeanza na unaendelea kwa kasi mkoani humo kuwa ni wa maji kutoka ziwa Victoria kwa ajili ya wakazi wa Wilaya za Nzega, Tabora na Igunga.

Miradi mingine ni ujenzi wa barabara za kiwango cha lami kuunganisha Mkoa huo na mikoa jirani ambapo ujenzi unaendelea.

Katika hatua nyingine wajumbe hao wamezitaka Halmashauri  za wilaya mkoani humo kuhakikisha kiasi cha fedha inachotenga kutokana na mapato ya ndani kwa ajili ya vijana, akinamama, walemavu na ile ya miradi ya Maendeleo zinatumika kama ilivyokusudiwa.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Ccm Mkoa Hassan Wakasuvi alisema kuwa asilimia kumi ya mapato ya ndani inayotengwa na kila Halmashauri kwa ajili ya makundi hayo ziwafikie walengwa bila kuwa na riba.

Alizitaka Halmashauri hizo kuweka utaratibu wa kupitia vikundi vyote vinavyopewa fedha hizo ili iweze kuvisaidia kukuza mitaji yao na waweze kuzirejesha zinufaishe wengine.

Aidha kikao hicho kiliwaagiza wajumbe wa Hamashauri kuu wa kila Wilaya kutembelea na kukagua miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao kutokana na fedha zinazotokana na asilimia 40 ya mapato ya ndani ya kila wilaya.

Hatua ilifikiwa baada ya kubainika baadhi ya Halamashuri za Wilaya zimekuwa zikiandika kwenye makaratasi kuwa zimetenga fedha  zilizotokana na mapato ya ndani kwa ajili ya miradi lakini hakuna kitu kilichofanyika.
  Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Janath  Kayanda akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa huo jana cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi akifungua Kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa huo jana cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ( wa pili kutoka kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi jana katika Kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi  CCM Mkoa wa Tabora.
 Baadhi ya Wajumbe wa Hamashauri Kuu ya Cahama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora wakiwa katika kikao maalumu jana kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. 
 Mbunge wa Urambo Margaret Sitta akiomba ufafanuzi jana wakati kikao maalumu jana Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele akitoa maoni yake jana wakati kikao maalumu jana cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. 
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora-Uyui Saidi Ntahondi akitoa maoni yake jana wakati kikao maalumu jana cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Picha na Tiganya Vincent

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad