HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 2, 2018

Mazao ya Chai, Kahawa, Mbogamboga pamoja na Matunda yapewa kipaumbele cha kuongeza thamani

Na Khadija Seif , Globu ya Jamii
SERIKALI  imepata msaada wa sh. Bilioni 265.5  kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya ya Chai, Kahawa, Mbogamboga  pamoja na Matunda.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutiliana saina na umoja wa Ulaya  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James amesema kuwa fedha hizo sio mkopo hivyo zitakwenda katika miradi iliyokusudiwa. Kutokana na vipaumbele vya fedha hizo.
James amesema msaada huo unatokana na miradi iliyofanyika kwa msaada wa umoja wa Ulaya kufanya vizuri na ndo maamna wamekuwa na imani na kutopa fedha kwa mara nyingine.

Amesema lengo  kuu mradi  wa kuboresha kilimo hicho ni  kukuza uchumi , kuimaraisha sekta binafsi na kuongeza ajira , Chakula na Lishe nchini.

Kipaumbele cha kwanza ni kutekeleza sera ya kilimo bora nchini ili kuongeza thamani ya Mazao ya Chai,Mbogamboga na Matunda ikiwa ni katika kuboresha barabara za vijijini katika maeneo ya utakapotekelezwa, uboreshaji wa sera ,sheria ,na mazingira ya biashara katika sektaa husika, kuendeleza mnnyororo thamani katika mazao ya Chai, Kahawa, Mbogamboga na Matunda, pamoja na kuongeza elimu na kuimarisha matumizi ya lishe bora.

Katibu Mkuu ofisi ya  waziri Mkuu sera na uratibu profesa Faustine Kamuzora ametoa shukrani kwa msaada huo wa fedha ambazo zitatumika katika vipaumbele vilivyoanishwa .

Kamuzora amesema wanakilimo wanakumbwa sana na changamoto ya miundombinu ya usafirishaji wa mazao  kwani imekua vigumu kisafirishwa  kwenda sehemu za mbali kutoka na barabara kuwa mbovu hivyo kupelekea mazao ambayo yanashindwa kuhimili hali ya hewa  inamlazimu kupeleka zao ambalo tayari limepoteza uhalisia wake.

Naibu Katibu Mkuu kutoka Zanzibar Hamadi Kassim Haji ametoa shukrani kwa kuendeleza  Kutuunga Mkono katika harakati za Maendeleo kwa Msaada wa euro 100.

 Haji amesema kwa upande wa Mji wa Zanzibar wamejikita Kwenye Kilimo cha chai na Mbogamboga na fedha hizi zimefika wakati ambao serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajipanga kuboresha Maendeleo kwa wakulima wa mazao mbalimbali.

Mkurugenzi wa shirika la EU ameeleza lengo la kusaidia fedha hizi ni kwa lengo la wakulima wadogowadogo japo hakuna ushirika wa wakulima kupitia serikali za mitaa itaweza kufikisha fedha hizo kwa vyama vya wakulima hao.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akitia saini makubaliano na Umoja wa Ulaya katika mradi uboreshaji mnyororo wa thamani katika mazao ya Kahawa, Chai, Mbogamboga  pamoja na Matunda
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akizungumza mara baadaya kutia saini ya msaada uliotololewa na Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuongeza thamani ya mnyororo wa thamani katika mazao Chai, Kahawa, Mbogamboga pamoja na Matunda katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini  Roeland Van De Gier akizungumza katika hafla ya kutiliana saini na serikali ya Tanzania ya utoaji wa fedha katika uboreshaji wa mnyororo wa thamani wa mazao ya Chai, Kahawa, Mbogamboga pamoja na Mtunda.
Picha ya pamoja Makatibu wakuu waliohudhuria utiaji saini, Balozi Umoja wa Ulaya  pamoja na wawakilishi wa Umoja huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad