BSS YANOGA KUPITIA STARTIMES - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 12 October 2018

BSS YANOGA KUPITIA STARTIMES

SHINDANO la kusaka vipaji vya muziki maarufu kama  BSS limeendelea kunoga kupitia StarTimes Swahili.

 Akizungumza na vyombo vya habari Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa amesema kuwa "kwa mara ya kwanza katika historia ya Bongo Star Search, itakuwa ikiruka kila siku kupitia chaneli yao ya Kiswahili, (ST Swahili) saa 3 Usiku, na hii ni kuwapa fursa ya  kutazama maudhui mengi zaidi ambayo wamekuwa wakiyakosa katika misimu iliyopita” ameeleza Malisa.

Imeelezwa kuwa shindano la Bongo Star Search limeingia katika msimu wake wa tisa baada ya mapumziko na mafanikio makubwa kwa misimu minane tangu kuanzishwa kwake. Pia ni shindano kubwa zaidi la vipaji kuwahi kufanyika nchini Tanzania, kwa mwaka huu shindano hilo linarushwa kupitia king’amuzi cha StarTimes na chaneli yao ya StarTimes Swahili ikiwa ni mara ya kwanza kwao kufanya hivyo.

“Tuna shauku kubwa sana kuwaletea maudhui haya ambayo kwa takribani miaka miwili watazamaji wa luninga wameyakosa, BSS ni shindano la kipekee na ambalo linaangaliwa na watu wa rika zote na hali zote, ndio maana sisi kama wafalme wa burudani za Kifamilia Tanzania tukaamua kulirudisha tena kwa ajili ya kila mmoja” amesema Malisa.

Afisa mahusiano wa Startimes Samwel Gisayi amesema kuwa  msimu huu kwa mara ya kwanza katika historia ya Bongo Star Search, vipindi vitakuwa vikiruka kila siku kupitia chaneli yao ya Kiswahili, (ST Swahili) saa 3 Usiku. Hii ni kuwapa fursa wateja wetu kutazama maudhui mengi zaidi ambayo wamekuwa wakiyakosa katika misimu iliyopita ambapo kipindi kilikuwa mara moja kwa wiki.

Usaili wa jijini Dar es Salaam katika kusaka vipaji hivyo unafanyika kwa siku tatu ili kuwapa nafasi watu wengi zaidi kushiriki katika shindano hilo na hii ni kwa kuzingatia idadi kubwa ya watu katika jiji hilo. 
Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa akizungumza na waandishi wa  habari leo katika usahili wa washiri wa kutafuta vipaji kupitia Bongo Star Search katika ukumbi wa Next Door jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad