HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 18 October 2018

BARAZA LA BIASHARA MKOA WA DODOMA LAASWA KUONGEZA USHIRIKI SEKTA BINFASI

Frank Mvungi- MAELEZO
MKUU wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge, ameongoza mkutano wa majadiliano ya Baraza la Biashara la mkoa huo ili kupitia na kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili usaidie kukuza ushiriki wa sekta binafsi na kuchochea ukuaji wa sekta zinatoa ajira kwa wananchi walio wengi kama kilimo.

Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo  leo Jijini Dodoma  na wadau wengine, Dkt. Mahenge amesema kuwa, mkutano huu una lengo la kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ngazi ya Mikoa na Wilaya.

“Tunategemea utakuwa rejea thabiti kwa viongozi na watendaji ambao wamekuwa wakibadilika mara kwa mara kutokana na uteuzi au chaguzi”. Alisisitiza Dkt. Mahenge

Akifafanua zaidi, mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma amesema mkutano huo wa majadiliano una lengo la kuhakikisha ushiriki wa sekta binafsi unaongozeka ili kuchochea maendeleo ya mkoa na taifa.

Aliongeza kuwa, majadiliano hayo yatasaidia kutatua changamoto zinazojitokeza mara kwa mara ambazo zimekuwa zikifubaza upatikanaji wa fursa za kiuchumi na kijamii na yanategemewa kutoa ufumbuzi wa changamoto  hizo kwa kuzingatia maandalizi ya majadiliano, kanuni za majadiliano na utekelezaji baada ya majadiliano.

“Ninatambua kuwa Mabaraza ya biashara yapo katika Wilaya zote mkoani hapa hivyo naamini yatatumika ipasavyo  na yatawezesha kuchochea Maendeleo katika Mkoa na Wilaya zetu kwa kushawishi ongezeko la biashara na uwekezaji”. Alibainisha Dkt. Mahenge.

Pia aliwahimiza  viongozi wa kisiasa na watendaji wote wahakikishe mabaraza ya biashara yanakuwa hai katika maeneo yao ili kuchochea maendeleo na ustawi wa wananchi.

Aidha, aliwataka viongozi katika ngazi za Wilaya kuboresha mazingira ya biashara yatakayowezesha wananchi  kutoa mchango kwenye pato la mkoa na taifa kwa ujumla.  

Michango ya wadau itakuwa imejumuishwa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa 10. Baada ya Mwongozo kukamilika utazinduliwa rasmi na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa tarehe itakayopangwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akifungua  mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  uliofanyika leo Jijini Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith akiteta jambo na Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa huo anayeshughulikia Sekta za Uchumi na Uzalishaji Bi Aziza Mumba mara baada ya mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  katika mkoa huo.
 Mhadhiri  kutoka  Chuo  kikuu  Mzumbe Prof. Honest   Ngowi akiwasilisha rasimu ya mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  wakati wa kikao cha kujadili muongozo  huo leo Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wakuu wa Wilaya wa mkoa wa Dodoma wakifuatilia mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  uliofanyika leo Jijini Dodoma.

 Sehemu ya washiriki  mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  uliofanyika leo Jijini Dodoma.

(Picha zote na MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad