HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 2, 2018

AIRTEL YAZINDUA MNARA WA MASAFA YA 3G MIKUMI, WATU ZAIDI YA ELFU 30 KUNUFAIKA WAKIWEMO WATALII

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua mnara wa mawaliano wenye uwezo wa kutoa huduma za Intanet kwa kiwango cha 3G kwa wakazi wa Kata ya Mikumi  ikiwa ni hatua ya Kampuni hiyo kurahisha huduma za masafa ya Mtandao kwa wateja wake na watalii wanaotembelea katika hifadhi ya taifa ya Mikumi.

Akizindua Mnara huo wenye uwezo wa kutoa huduma za mtandao kwa masafa ya 3G Diwani wa kata ya Mikumi Rivinus Mwawira amesema, Mbali na upatikanaji wa Masafa ya Mtandao lakini pia wakazi wake Zaidi ya elfu 30 watapata fursa mbalimbali za kimaendeleo kama kutuma na kupoke fedha kwa urahisi na pia huduma ya mawasiliano ya kawaida ya simu za mkononi.

“Mimi na wananchi wangu wa Mikumi tumekuwa na shauku kubwa ya kupata manara huu, lakini jambo kubwa zaidi ni upatikanaji wa Masafa ya 3G kwani utaturahisishia sana kazi zetu kwani ukiwa na Internet ya uhakika kila kitu kinakua rahisi”Amesema bw Mwawira

“Manufaa Mengine yanayopatikana kutokana na uwepo wa Mnara huu hapa kwetu ni pamoja na wanafunzi kujisomea kwa kutumia program mbalimbali zinazopatikana mtandaoni ikiwa ni pamoja na Masomo ya Ufundi ya VSOMO inayotolewa kwa ushirikiano baina ya Airtel na VETA” Amesisitiza Diwani huyo

Kwa upande wake Meneja mauzo wa Airtel Kanda ya Morogoro Gibson Renatus alielezea kuwa manufaa yanayopatikana baada ya kuzinduliwa kwa mnara huo katika eneo la mikumi ni pamoja na upatikanaji wa mawasiliano ya simu za mkononi, Huduma ya Airtel Money na huduma bora za mtandao za 3G.

Baadhi ya Wananchi wa eneo la Mikumi wameelezea furaha yao baada ya kuboreshwa kwa mfumo wa mawasiliano wa kampuni ya Airtel katika eneo lao.

“Sasa hivi tunaweza kutuma na kupokea fedha kwa urahisi kupitia Airtel Money, tunapata internet yenye kasi ya 3G na pia hatupati tabu kupiga na kupokea simu tukiwa popote ndani nan je ya eneo letu la Mikumi” walieleza wananchi hao

Kuzinduliwa kwa mnara huo wenye uwezo wa kutoa huduma za mawasiliano na mfumo wa Internet wa 3G utawawezesha wakazi Zaidi ya elfu 30 wa kata ya mikumi na maeneo ya jirani kutuma na kupokea fedha, kuwa na mawasiliano ya uhakika wakati wote, kutumia internet kupakua na kupakia taarifa mbalimbali na hivyo kurahisha shughuli zao za kila siku.

Diwani wa Kata ya Mikumi Rivanus Mwawira akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa kampuni ya simu ya Airtel  wenye uwezo wa kutoa huduma za mawasiliano ya kawaida na masafa ya internet ya 3G katika eneo la Mikumi, Wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Wanaoshuhudia ni Meneja Mauzo wa Airtel Mkoa wa Morogoro Gibson Renatus mwenye Fulana Nyekundu na Maofisa wa serikali ya mtaa na kitongoji cha Mikumi Mjini
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Jackson Mmbando akitoa ufafanuzi kwa Diwani wa kata ya Mikumi Rivanus Mwawira mwenye Suti na Maofisa wengine wa serikali na watendaji wa kampuni ya  Airtel wakati wa hafla ya uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wenye uwezo wa wa kutoa huduma ya masafa ya 3G katika eneo la Mikumi, wilayni Kilombero mkoani Morogoro hivi karibu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad