Na Anitha Jonas – WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka vijana wote wa kitanzania waliohitimu Shahada katika vyuo vikuu nchini kujitokeza na kwenda Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa ajili ya kupata mafunzo yatakayowasaidia kuwa walimu wa lugha ya Kiswahili kwa wageni kutokana na wataalamu wa lugha hiyo kusuasua kujiandikisha katika kanzi data ya wataalamu wa hiyo.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga mafunzo ya wataalamu wa lugha ya Kiswahili yaliyoandaliwa na BAKITA kwa ajili ya kuwajengea Ustadi wataalamu ya Kiswahili ili waweze kufundisha wageni lugha ya Kiswahili.
“Mpaka sasa nimepewa takwimu za wataalamu tisini na sita wa lugha ya Kiswahili nchini ambao ndiyo waliyojitokeza waliyojitokeza kujiandikaisha katika kanzi Data ya waatalamu wa lugha hii,kwa kweli sijui ni kwanini watanzania wanakuwa wazito katika kuchangamkika fursa badala yake mambo yakibadilika wataanza kulalamika,kwani lengo la kanzi data hii ni kurahisisha mfumo wa kuwafikia wataalamu wa lugha hii kwa haraka pale fursa zinapo kuja,”alisema Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika sherehe za kufunga mafunzo hayo Waziri huyo mwenye dhamana na masuala ya lugha nchini alieleza kuwa kwa sasa kuna uhitaji mkubwa wa wataalamu kwa ajili ya kufundisha lugha ya Kiswahili na tayari kuna maombi yamesha kwisha wakilishwa kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Sudani Kusini, Rwanda na Afrika ya Kusini kwajili ya kupatiwa waatalamu wa lugha ya Kiswahili na wataokweda kufundisha katika nchini hizo.
Kwa upande wa Katibu Mtendaji BAKITA Dkt.Selemani Sewangi alimpongeza mheshimiwa Waziri Mwakyembe na kumweleza kuwa taasisi hiyo hivi karibuni inatarajia kuanza kutoa mafunzo ya ukalimani na wanatoa wito kwa watanzania wote na wataalamu wa lugha wanaoona kuwa wanauwezo wa kuwa wakalimani wa lugha mbalimbali wafike katika ofisi yao kwa ajili ya kupata mafunzo.
“Kwa sasa lugha ya Kiswahili siyo lugha ya Tanzania pekee bali ni lugha ya Afrika nzima na kama tafiti zinavyoonyesha ifikapo mwaka 2063 bara zima la Afrika litakuwa linaongea lugha hii vizuri hivyo ni vyema kuongeza jitihada za kutosha kwa wataalamu wa lugha hii kwa lengo la kuikuza vyema tukiwa kama watumiaji wa kwanza wa lugha hii barani Afrika,”alisema Dkt.Sewangi.
Pamoja na hayo nae Mkufunzi wa lugha ya Kiswahili kwa Raia wa Marekani wanaokuja nchini kwa ajili ya shughuli za kujitolea Bw.Majid Mswahili alialiwataka wakufunzi hao waliyotunikiwa vyeti baada ya kumaliza masomo yao kuhakikisha wanakwenda kuifanya kazi hiyo ya kutoa elimu ya lugha ya Kiswahili kwa wageni kwa weledi ili kuonyesha umahiri wa watanzania katika lugha hiyo.
Hata hivyo nae mmoja ya wahitimu wa mafunzo hayo ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kufundisha wageni Bi.Janeth Ngowi aliipongeza serikali kwa jitihada zake za kupambana kuhakikisha lugha ya Kiswahili inapewa heshima ndani na nje ya nchi na pia kwa kuanzisha Kanzi Data ya Kiswahili nchini kwa hii itasaidia kutoa ajira kwani lugha hii adhimu niya kujivunia.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe
(katikati)akizungumza na wahitimu wa mafunzo ualimu wa lugha ya
Kiswahili kwa wageni yaliyokuwa yanatolewa na Baraza la Kiswahili
Tanzania (BAKITA) leo Jijini Dar es Salaam katika sherehe ya kuwakabidhi
vyeti wahitimu wa mafunzo hayo,kutoka kulia ni Katibu Mtendaji BAKITA
Dkt.Selemani Sewangi.
Katibu
Mtendaji Baraza la Kiswahili Tanzania Dkt.Selemani Sewangi (kulia)
akimweleza Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Dkt.Harrison mwakyembe mchakato wa taasisi hiyo wa kuanzisha programu ya
mafunzo ya ukalimani hivi karibuni leo jijini Dar es Salaam wakati wa
Sherehe ya kuwakabidhi vyeti walimu wa lugha ya Kiswahili kwa wageni
baada ya kumaliza mafunzo yao.
Mmoja
wa wahitimu wa Mafunzo ya ualimu wa Lugha ya Kiswahili kwa wageni
ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na
mwanafunzi wa PHD katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mwl.Editha Adolf
akisoma shairi la kusifu lugha ya Kiswahili mbele ya Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo
pichani) katika sherehe ya kuwa kabidhi vyeti wahitimu hao iliyofanyika
leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe
akimkabidhi cheti Mwalimu Prisca Mihayo kutoka Shule ya Sekondari Meli
Mkoa wa Kilimanjaro leo jijini Dar es Salaam katika sherehe ya kukabidhi
vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ualimu wa lugha ya Kiswahili kwa
wageni yaliyokuwa yanatolewa na Baraza la Kiswahili la Tanzania.
Waziri
wa Habari Utamdauni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe
akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya ualimu wa lugha
ya Kiswahili kwa wageni mara baada ya kuwakabidhi vyeti vyao vya
kuhitimu mafunzo hayo yaliyokuwa yanatolewa na Baraza la Kiswahili
Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment