HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 21 September 2018

WAVUNDI VINAVYOPOKEA MSAADA WAASWA KUSIMAMIA KIDETE

VIKUNDI vilivyopokea msaada kutoka Mfuko wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania vimeshauriwa  kusimamia kidete ili fedha zinazotolewa zifanye kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo.

Hayo yamesemwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Immi Patterson amesema kuwa fedha hizo zitumike katika kutokomeza unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.

Akizungmza jijini Dar es Salaam leo Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Immi Patterson wakati wa kugawa vyeti vya kufanikisha kupata msaada uliotolewa na Mfuko wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.

 amesema kuwa wanufaika wa msaada walituma maombi ya kupata fedha hizo zinazotoka katika mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na UKIMWI(PEPFAR) ikiwa ni mwitikio wa maombi ya kuwasilisha maandiko ya miradi inayolenga kusaidia miradi ya vikundi hapa nchini.

"Kwa mara ya kwanza katika historia ya zama za sasa tumepata fursa ya kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi bila chanjo". Amesema Immi Patterson.

Amesema kuwa jitihada za sisi sote zitasaidia kufika pale tunapotaka katika jitihada za kutokomeza Ukimwi hapa nchini.
Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Immi Patterson akizungumza na wanavikundi wanaosaidia mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI jijini Dar es Salaam leo.  

  
 Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Immi Patterson akitoa vyeti vyeti kwa wanavikundi ambao mfuko wa balozi wa Marekani wa kusaidia mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI unaosaidia makundi ya kijamii na watu waishio na virusi vya ukimwi kushughulikia Changamoto zao vikundi vilivyopo mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Immi Patterson akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa vikundi 19 ambavyo vitasaidia kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad