HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 13, 2018

WATUMISHI WA UYUI WAPEWA MWEZI MOJA KUTOKA TABORA NA KWENDA KUISHI ISIKIZYA

Na Tiganya Vicent
SERIKALI ya Wilaya ya Uyui imesema itawachukua hatua watumishi ambao hadi kufikia mwisho wa mwezi huu (Septemba) watakuwa bado hawajahamia katika eneo la Isikizya na kuacha kuishi Tabora mjini.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(Uyui).

Alisema haiwezekani Halmashauri hiyo imenunua nyumba kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika eneo hilo lakini ni watumishi wachache ndio wanaoishi katika nyumba hizo na kuzifanya zile ambazo hazikaliwi kuanza kuchakaa.

Msuya aliongeza kuwa watumishi wamekuwa wakitumia gharama kubwa ya nauli ya kwenda na kurudi Tabora mjini kwa sababu ya nauli na wakati mwingine kuchelewa kazini.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kitendo cha watumishi hao kukaa nje ya kituo chao cha kazi ni kosa na kinapunguza ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi ambao kodi zao ndio zinatumika kuwalipa mshahara.

Alisema itakapofika mwisho mwa Mwezi huu mtumishi yoyote ambaye ataendelea kukaa Tabora mjini atakuwa amekaidi na hatua dhidi yake zitachukuliwa kwa mujibu taratibu na Sheria za utumishi wa umma.

Msuya alisema kuwa mtumishi wa aina hiyo atahesabika kuwa nje ya kituo chake cha kazi bila taarifa za Mwajiri wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad