Na Emmanuel Massaka,Global ya jamii
WILAYA ya Mkuranga ni moja ya wilaya saba zilizopo mkoani pwani wakazi wake wakijishughuisha sana na shughuli za kilimo ilikujipatia kipato.
Wilaya ya Mkuranga inalima mazao mbalimbali ya biashara na ya chakula ikiwemo Mihogo,Mbaazi, ,Korosho Machungwa Ufuta Mananasi pamoja na Nazi.
Pia wananchi wa Mkuranga wanategemea sana kilimo katika uchumi wao ambapo moja ya zao lililoshika kasi ni korosho,wanasomesha watoto kupitia korosho pamoja na kukuza pato la mtu mmoja mmoja.
Akizungumza wilayani Mkuranga mkoani Pwani Umri Manage mkulima wa mihogo na bamia alisema kuwa kilimo kimemsaidia kwani ndio kinachoendesha Maisha yake"mimi nalima bamia linaniongezea kipato changu cha kila siku pia namsaidia mume wangu baadhi ya majukumu"alisema.
Manage alitoa wito kwa wanawake wote nchini kuacha kujibweteka na kuacha utegemezi masala yake wajishughulishe katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mfanyabiashara na Mkulima wa Bamia,Umri Manage akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana Kilimo.
Wananchi wakivuna Mihogo kama walivyokutwa na kamera yetu
Wananchi wa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani wakivuna Mihogo kama walivyokutwa na kamera yetu.
Picha na Emmaniel Massaka wa Global ya jamii)
Picha na Emmaniel Massaka wa Global ya jamii)
No comments:
Post a Comment