HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 10, 2018

HALMASHAURI YA MKURANGA YARUDISHA ENEO LA DUNDANI

HALIMASHAURI ya Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani imelirudisha eneo la Dundani ililolichukua kwa madhumuni ya kufanya shughuli za uwekezaji wa viwanda na kulirudisha mikononi mwa wananchi.

Eneo lililorudishwa ni lenye ukubwa wa hekari 325 ambalo lilifanyiwa utahmini kati ya hekari 700 zilizochukuliwa na Halmashauri hiyo kwa lengo la kulifanya kuwa eneo la uwekezaji.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Dundani, ambao maeneo yao yalichukuliwa na Halmashauri hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga alisema kuwa nia ya serikali ilikuwa njema sana na sulala hilo liliangaliwa kwa umakini na viongozi wa Halmashauri hiyo.

Aidha alisema kwua viwanda vingi vilivyojengwa  katika wilaya hiyo vilijengwa kiholela hivyo kusababisha usumbufu na madhara kwa wakazi wa maeneo hayo ikiwemo kutiririsha maji machafu ya viwandani na kukosa njia za kupita.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema Ofisi yake kwa kushirikiana na kamati teule ya wananchi wenye maeneo na wataalamu waliopo ofini kwake wataandaa barua ambayo itakabidhiwa kwa wenye maeneo kabla ya mwisho wa mwezi Septemba.

Sanga alisema serikali wilayani humo iliamua kulichukua eneo hilo ili kuepuka uwekezaji holela uliokuwa ukifanyika kwa kasi kutokana na wamiliki wa maeneo hayo kuyauza kwa kasi, kasi ambayo anasema hata hivyo kwa sasa imepungua sana.
Hata hivyo aliwaomba wamiliki wa eneo hilo kuepuka uwekezaji  wa kiholela pale watakapokabidhiwa rasmi maeneo yao.


Awali alijitokeza Muwekezaji kutoka nchini Misri aliyefika kaetika eneo hilo na kuahidi kurudi lakini hakufanya hivyo kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo mnamo mwaka 2014/2015.
Mwekezaji mwengine alitoka nchini China, yeye alitaka kuwepo kabisa miundombinu ya bara bara na umeme  vitu ambayo hata hivyo ilikuwa ngumu kwa serikali kwa sababu hata fidia ilikuwa haijatolewa kwa wenye maeneo.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Mhandisi Mshamu Munde alisema kuwa fidia ya kuwalipa wamiliki wa eneo hilo ni kiasi cha shilingi bilioni 7.9 huku mapato ya ndani ya Halmshauri kwa mwaka ni shilingi bilioni 3.8 hadi 4.3.
Mkurugenzi anasema awali wananchi walifikiri halmashauri ingekopa na kisha kuwafidia lakini hiyo suala hilo lisingewezekana kutokana na ufinyu wa mapato ya halmashauri.
akielezea matumizi ya mapato hayo ya ndani ambayo yanatokana na bidhaa za madini ikiwemo mchanga, bidhaa za kilimo, korosho, ufuta na bidhaa za misitu na ushuru wa viwandani.
matumizi ya wilaya hiyo ni pamoja na asilimia kumi kwa (Wanawake, vijana na walemavu), asilimia 60 inaenda miradi ya amendeleo vijijini, asilimia 20 mgao wa vijijini, asilimia 10 inatumiwa kwenye ufuatiliaji huku Akiba inayobaki ndio pengine ingelipa mkopo ambayo isingewezekana.

Akizungumzia uamuzi huo wa seikali Said Mohamed, mmoja wa wamiliki wa eneo hilo alisema uamuzi wa serikali hakuridhsiwa nao kwa vile maeneo hayo yamechukuliwa muda mrefu na kuahidiwa kulipwa fidia lakini leo wanaelezwa kuwa watarudishiwa.
Sande kauli imemvunja moyo na kumkatisha tamaa sababu wakati maeneo hayo yalipokuwa yanachukuliwa hakupenda, lakini kwa ushawishi wa serikali alikubali na kuahidiwa kulipwa Fidia baada ya miezi sita lakini sasa zaidi ya miaka minne wanaambiwa kuwa wanarudishiwa Ardhi kwa asilimia 100 hajafurahishwa nao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad