HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 10, 2018

BODI YA KOROSHO YASHAURIWA KUZITUMIA TAASISI ZA KIJESHI ZA JKT MGAMBO NA JKT MARAMBA MCHAKATO WA UZALISHAJI WA MICHE YA KOROSHO

 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la korosho uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya Tasnia ya zao la korosho kwa kipindi cha msimu wa miaka mitatu katikati ni  Meneja Bodi ya korosho Kanda ya Kaskazini Mashariki Ugumba Kilasa na kulia ni Mrajisi Msaidizi vyama vya Ushirika Mkoa Tanga Jacklin Senzige
 Meneja Bodi ya korosho Kanda ya Kaskazini Mashariki Ugumba Kilasa katika mkutano huo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
 Mrajisi Msaidizi vyama vya Ushirika Mkoa Tanga Jacklin Senzige akizungumza kwenye mkutano huo

 MKUU wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza katika mkutano huo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Gwakisa Kasongwa akizungumza katika mkutano huo kuliaa ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Gwakisa Kasongwa katikati akiwa na wakuu wa wilaya wa wilaya za Kilindi Sauda Mtondoo kushoto kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa anayaafuata ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark wakifuatilia kwa umakini mkutano huo
 Wwenyeviti wa Halmashauri mbalimbali mkoani Tanga wakiwa kwenye mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani Seif Ally
 Baadhi ya wakurugenzi wakifuatiliaa mkutano huo
 Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba kushoto akisisitiza jambo kwenye mkutano huo
BODI ya korosho Mkoa Tanga imeshauriwa kuzitumia taasisi za Kijeshi za JKT Mgambo na JKT Maramba ili ziweze kusaidia katika mchakato wa uzalishaji wa miche ya mimea hiyo ya korosho.

Hayo yamezungumzwa  na Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella kwenye mkutano wa wadau wa zao la korosho uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya Tasnia ya zao la korosho kwa kipindi cha msimu wa miaka mitatu.

Shigella alisema ili bodi hiyo iweza kukabiliana na uhaba wa miche katika Halmashauri zinazolima zao hilo lazima ifike wakati taasisi hizo ziweze kutumika kukabidhiwa mbegu kwa ajili ya kuzalisha miche hiyo.

“Jaribuni kuwasiliana na taasisi hizio za kijeshi ambazo wanawataalamu wa kuandaa vitalu wanaweza kuwasaidia kuzalisha miche mingi na iliyo na ubora unaotakiwa”Alisema Shigella.

Mbali na hilo pia alizitaka Halmashauri zote zinazolima zao hilo kuhakikisha zinatenga bajeti mapema ndani ya mwezi huu wa Sept kwa ajili ya ununuzi wa mbegu toka katika Taasisi ya Utafiti wa kilimo(Naliendele) kwa ajili ya uzalishaji wa miche ambayo inatarajiwa kusambazwa mwakani kwa wakulima wote

Awali akizungumzi suala hilo Meneja Bodi ya korosho Kanda ya Kaskazini Mashariki Ugumba Kilasa alikiri umuhimu wa kuzitumia taasisi hizo kutokana na na uhaba wa fedha zilizokuwa zinatumika kuvilipa vikundi vinavyozalisha miche hiyo.

Kilasa alisema lengo ni mjadala wa kuongeza uzalishaji wa zao hilo Mkoani hapa na ongezeko hilo lazima liendende sambamba na uwepo wa miche mipya,bora na ya kisasa jambo ambalo ikiwa kutaanzishwa vitalu vya kukuzia miche na taasisi hizo hali ya uzalishaji inaweza kubadilika.

“Awali tulikuwa na vikundi vya vijana tuliokuwa tunawatumia kuzalisha miche hiyo na tulikuwa tunawalipa lakini kutokana na ufinyu wa fedha ni bora tutumie taasisi hizo za JKT zitatusaidia”Alisema Kilasa.

Alisema mikakati endelevu ifanyike ili kuhakikisha ongezeko la uzalishaji linakuwepo hasa kwa kupanda miche mipya itakayoweza kuzaa kwa wingi na kuongeza uchumi wa mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla

Nae Mrajisi Msaidizi vyama vya Ushirika Mkoa Tanga Jacklin Senzige alisema kweli lipo tatizo la upatikanaji wa pembejeo kwa wakati jambo ambalo linaweza kukwamisha usambazaji wake kwa wakulima na kuathiri uzalishaji kwa ujumla.

Alisema uzalishaji wa Korosho mkoani Tanga umeshuka kutoka tani 1712 mwaka 2016/2017 hadi kufikia tani 1381 mwaka 2017/2018 hali iliyosababishwa na mvua za mfululizo zilizonyesha kwa kipindi kirefu na kusababisha maua kudondoka na kuozesha matunda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad