Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde akizungumza na mwenyekiti wa UVCCM Mjini Kibaha Azilongwa Bohari(kulia ) wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yaliyoandaliwa na umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kibaha ,katika ukumbi wa mikutano wa shirika la elimu Kibaha .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde akizungumza wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yaliyoandaliwa na umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kibaha ,katika ukumbi wa mikutano wa shirika la elimu Kibaha .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde akikabidhiwa mpango kazi na mwenyekiti wa UVCCM Mjini Kibaha ,Azilongwa Bohari .(picha na Mwamvua Mwinyi)
NA MWAMVUA MWINYI ,KIBAHA
SERIKALI imeanzisha mpango wa kurasimisha ujuzi kwa vijana ambao hawajapata mafunzo kwenye vyuo licha ya kuwa na vipaji vya ufundi mbalimbali.
Aidha amewataka vijana wa Mji wa Kibaha ,mkoani Pwani kuchangamkia fursa ya ujasiriamali pamoja na ajira kupitia uwekezaji wa viwanda mkoani humo kwa lengo la kujiinua kimaisha
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde alitoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yaliyoandaliwa na umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kibaha ,katika ukumbi wa mikutano wa shirika la elimu Kibaha
Alisema ,mpango huo utakamalizika 2021 utawatambua vijana hao ambao hawajawahi kupata mafunzo kwenye vyuo vya ufundi na tayari wameomba vijana 22,000 nchi nzima ambapo wenye sifa ni 14,311 pekee.
Mavunde alisema kuwa , awamu ya kwanza imeanza na vijana 3,900.
Alieleza, mpango huo utafanywa na vyuo vya ufundi Veta ambao wanakwenda mtaani na kuwaangalia vijana na kurekebisha mapungufu na kuyatatua ndani ya wiki ama mwezi na wakimaliza wanawapa vyeti vya ufundi.
Alisema , waliomaliza wameanza kupata ajira kwenye kampuni za ujenzi.
“Upo mradi mwingine unaofadhiliwa na shirika la misaada la Marekani na vijana 30,000 kwenye mikoa ya Iringa,Mbeya na Zanzibar wanasomeshwa na serikali"alisema Mavunde.
Hata hivyo ,Mavunde aliwasihi vijana kuunda vikundi na makampuni katika kufanya shughuli za kiuchumi na pia kupata fursa ya uwezeshwaji na mifuko ya serikali.
Nae mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Pwani ,Charangwa Makwiro alieleza, mikakati ya kuwakwamua vijana kiuchumi kupitia kilimo na kuahidi kwamba watausimamia kwa dhati utekelezaji wa mkakati huo ili kuwaletea maendeleo ya vijana wa mkoa huo.
Awali mwenyekiti wa UVCCM Kibaha Mjini Azilongwa Bohari alisema, wameamua kufanya mafunzo hayo ili vijana waweze kutambua fursa zilizopo na namna ya kuweza kuvifikia.
Alisema tayari UVCCM wilayani hapo wamepata maeneo ambayo watafanya shughuli za kilimo na ufugaji.
Azilongwa aliwataka, vijana kushiriki katika mradi huo ambao utasaidia kupunguza hali ya kuwa tegemezi na kujiajiri wenyewe ili kujiongezea kipato.
Katika mafunzo hayo ,baadhi ya vijana hao walichangia benki ya damu ya hospitali ya rufaa ya mkoa ya Tumbi ambapo zilipatikana unit 20.
No comments:
Post a Comment