HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 27, 2018

VAN VICKER ATUA NCHINI KWA AJILI YA UZINDUZI WA FILAMU YA D.A.D

Muigizaji wa Kimataifa wa Nchini Ghana Van Vicker  akizungumza  mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa JKNIA kwa ajili ya uzinduzi wa filamu mpya ya D.A.D aliyoshirikishwa na muigizaji wa Tanzania Wema Sepetu utakaofanyika kesho Septemba 28  katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


MUIGIZAJI wa Kimataifa wa Nchini Ghana Van Vicker ametua nchini kwa ajili ya uzinduzi wa filamu mpya ya D.A.D aliyoshirikishwa na muigizaji wa Tanzania Wema Sepetu utakaofanyika kesho Septemba 28  katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Van Vicker ametua Tanzania alfajiri ya leo kwa ajili ya uzinduzi wa filamu hiyo iliyotakiwa izinduliwe miaka mitatu iliyopita, sasa inazinduliwa Septemba 28, 2018 siku ambayo Wema atakuwa akitimiza umri wa miaka 30.


Msanii huyo kutoka Ghana amepokelewa na mwenyeji wake  Wema Sepetu pamoja na wasanii wengine tayari kabisa kwa ajili ya kuzindua filamu hiyo baada ya kushindikana kufanyika Juni 30 kwa Van Vicker kushindwa kuwasili kusema hatahudhuria kutokana na kubanwa na shughuli nyingine.


Wema Sepetu amezungumza baada ya kuwasili kwa muigizaji huyo, amesema Van Vicker ni rafiki yake lakini kwa muda mrefu amekuwa akishindwa kufanikisha uzinduzi huu mara nyingi akidai yupo bize na kazi zingine,.

“Van Vicker ni rafiki yangu lakini hapo katikati tumekuwa tukikwaruzana mara kwa mara kwa sababu kila nikimwambia filamu inabidi iingie sokoni mara ataniambia hivi mara vile, lakini siku zote alikuwa ananiambia anataka tufanye kitu kizuri,” alisema.


Kukutana kwa Wema Sepetu na Van Vicker ilikuwa ni baada ya kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi katika mtandao wa Instagram akimuomba wafanye kazi pamoja na baada ya muda mfupi alimjibu hata yeye angefurahi kufanya kazi naye.

“Baada ya kumtumia ujumbe mfupi alinipa namba yake ya simu, tulizungumza namna tutakavyofanya kazi, kwa sababu nilitaka kufanya kazi kimataifa nilimwambia lazima niende Ghana akakubali. Nakumbuka nilikaa wiki mbili kule wakati wa kutengeneza filamu hii.”

Uzinduzi wa filamu hiyo iliyobatizwa jina la D.A.D unakuja miaka mitatu tangu walipoigiza huku Wema akisema Mghana huyo ndio chanzo cha kuichelewesha kuingia sokoni kwa kuwa amekuwa na mambo mengi kiasi cha kuwafanya wakwaruzane mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad