HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 27, 2018

HUU NDIO UJUMBE WA CHIKI KWA WASANII WANAOCHIPUKIA

Khadija Seif, Globu ya jamii
STAA mwenye ubora wake katika tasnia ya filamu za kibongo a.k.a Bongo Muvie  Chiki Mchoma amewashauri  wasanii  wanaochipukia kuhakikisha wanaishi maisha yao halisi.

Amesema hata yeye pamoja waigizaji wengine wengi wakongwe wameishi maisha ya kawaida na kujenga heshima kwa wadau.

 Chiki amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anapiga stori na Micbuzi Blog ambayo imekutana na Staa huyo na kuzungumza mambo kadhaa kuhusu sanaa ya uigizaji nchini.

Amesema changamoto inayowakumba kwa sasa wasanii chipukizi  ni kutopitia makundi mbalimbali ya filamu kama vile zamani wasanii ambavyo wamepitia na  kujifunza vingi kuhusu uigizaji.

Amefafanua kupitia makundi hayo waigizaji wengi wamepata  elimu, uzoefu pamoja na tabia  njema na matokeo yake wamejijengea heshima katika jamii na tasnia ya filamu kwa ujumla.

Pia Mchoma amesema kuna baadhi ya  wasanii kwa sasa wanaishi kwa kutegemea kiki wakiamini ndio zinaweza kuwapatia umaarufu badala ya kuweka jitihada kwa  kutengeneza kazi nzuri.

Ameongeza uzoefu wao ndio umeweza kuwajenga hivyo basi wajitahidi kujenga heshima ili waheshimike kwa watazamaji pamoja na wadau wa filamu.

"Kwa mataifa ya nje msanii akifanya jambo ambalo halipendezi kwa jamii anachukuliwa hatua kali tofauti na hapa kwetu linachukuliwa ni jambo la kawaida," amesema.
  
Amewataka  wanahabari waelekeze nguvu nyingi kwenye kutangaza kazi zao kuliko kuwatengenezea chuki baina ya msanii kwa msanii au kikundi fulani cha watu.

Ametoa mwito kwa wasanii  wanaotegemea Kiki kuwa  hazitawajengea chochote  badala yake zitafanya wanajamii kuiga mambo ambayo yatawapotosha kwani wasanii ni kioo cha jamii .

Na kwamba chochote watakachokifanya wapo watu ambao wanawatazamaa au  kuyafata.
Msanii wa filamu nchini, Chiki Mchoma akizungumza na Michuzi Blog kuhusu  wasanii chipukizi kusema jitihada    zao katika kazi ili watengeneze kazi nzuri na kufikia malengo waliyojiwekea.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad