HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 13, 2018

TIGO YAZINDUA MTANDAO WA 4G+ TANZANIA

Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali Tigo Tanzania, leo imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za mtandao wenye kasi ya juu zaidi nchini baada ya kuzindua teknolojia ya 4G+. 

Uzinduzi wa mtandao wa 4G+ unathibitisha kuwa Tigo ni kampuni pekee ya mawasiliano inayofanya ubunifu unaoboresha huduma zake kuendana na mahitaji halisi ya wateja nchini kote. 

‘Uzinduzi wa  4G+ ni sehemu ya safari ya mabadiliko ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo hapa nchini. Lengo letu ni kuwawezesha wateja kufurahia huduma bora zaidi za kidigitali. Daima tuko mbele katika kuleta teknologia za kisasa za mawasiliano nchini,’ Afisa Mkuu wa Tigo – Teknologia na Mawasiliano Jerome Albou aliwaambia waandishi wa habari katika uzinduzi wa mtandao wa Tigo 4G+ jijini  Dar es Salaam.  

Sasa wateja wa Tigo wanaweza kufurahia huduma bora, za uhakika na zenye kasi ya juu zaidi ya kupakua maudhui kutoka kwenye mtandao kwa gharama zile zile. Ili kufurahia mtandao wa 4G+, mteja anahitaji kuwa na simu yenye uwezo wa 4G+. 

Teknologia ya kisasa ya Tigo 4G+ inaongeza wigo wa matumizi ya huduma za kidigitali nchini. Teknologia hii inapanua utoaji wa huduma za intaneti yenye kasi ya juu zaidi, pamoja na kutoa huduma za sauti zinazoendana na mabadiliko ya maisha. 

‘Kampuni yetu inajivunia kuzindua teknolojia ya 4G+ inayoiweka Tanzania katika ramani ya teknolojia ya mawasiliano duniani. Sasa tunashindana na nchi zilizoendelea ambazo tayari zinawekeza katika teknolojia ya 5G. Kupatikana kwa teknolojia ya kisasa ya mawasiliano nchini Tanzania kunaibua fursa mpya za matumizi ya mtandao kwa wateja wetu,’  Afisa Mkuu wa Biashara - Tigo, Tarik Boudiaf alibainisha.   

Mbali na kujivunia mtandao wa 4G ulionea katika miji 22 nchini, mtandao wa Tigo 4G+ tayari unapatikana katika miji ya; Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Moshi na Dodoma, hata hivyo mipango ya kuendelea kuupanua mtandao huo kufikia miji mingine zaidi nchini inaendeliea.  Wateja wanaotumia simu zenye uwezo wa 4G+ sasa wanaweza kufurahia kasi ya juu zaidi ya kupakua maudhui mbali mbali kwa gharama zile zile za intaneti. 

Mtandao wenye kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+ una kasi mara mbili ya ule wa Tigo 4G, kwani Tigo  4G ina kasi ya 60Mbps ilihali mtandao mpya wa Tigo 4G+ unaweza kufikia kasi ya hadi 120Mbps. Kwa ujumla, wateja wanaotumia Tigo 4G+ katika eneo husika hugawana kasi hii ya juu zaidi miongoni mwao.

Katika juhudi za kuboresha na kupanua huduma za kidigitali nchini, Tigo ilikuwa mojawapo ya kampuni za mawasiliano za kwanza kabisa kuwekeza katika teknolojia ya 3G na  4G ambapo Tigo ndio kampuni pekee yenye mtandao mpana zaidi wa 4G nchini. Tigo pia ilikuwa ya kwanza kuzindua simu janja yenye lugha ya Kiswahili pamoja na huduma ya Facebook kwa lugha ya Kiswahili iliyoongeza matumizi ya huduma za kidigitali kwa idadi kubwa ya Watanzania wanaotumia lugha ya Kiswahili kwa mawasiliano yao ya kila siku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad