Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (kulia), akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wafanyakazi wake kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti jijini Dar es Salaam leo kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF).
Meneja Huduma za Jamii wa Barclays Tanzania, Hellen Siria (kulia), akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wafanyakazi wake kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti jijini Dar es Salaam leo kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF).
Mshauri na mtaalamu wa masuala ya afya magonjwa ya saratani, Dk. Dominista Kombe (kulia) akionyesha jinsi ya kuangalia viashiria vya ungonjwa wa saratani ya matiti kwa baadhi ya wafayakazi wa Benki ya Barclays katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF), jijini Dar es Salaam leo.
Mratibu kutoka Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF), Kisa Mwakatobe (kulia), akizungumza katika semina iliyoandaliwa na benki ya Barclays kwa wafanyakazi wake kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti jijini Dar es Salaam leo kwa kushirikiana na taasisi hiyo.
Mmoja wa waratibu kutoka Taasisi ya Saratani ya Matiti Tanzania (TBCF), Gloria Kida (kulia), akitoa ushuhuda wake wa jinsi alivyougua ugonjwa huo pamoja na matibabu aliyoyapata wakati wa semina hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barclays wakihudhuria mafunzo hayo kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa saratani ya matiti jijini Dar es Salaam leo.
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya saratani
nchini Dk.Dominista Kombe amesema saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoongoza
kwa kuua na kwamba kwa siku wagonjwa 80 wa aina mbalimbali za saratani hufariki dunia.
Ameishauri jamii na hasa wanawake kujenga utamaduni wa kupima afya zao
mara kwa mara ili kutambua iwapo wana tatizo la saratani au la huku akifafanua
changamoto kubwa wagonjwa wengi wanafika hospitali wakiwa wamefikia hatua ya tatu
au ya nne.
Dk.Kombe ambaye kwa sasa ni mstaafu na
ameamua kuanzisha Dar es Salaam Oncological Care Clinic amesema hayo leo wakati
anazungumza na wafanyakazi wa Benki ya Barclays kabla ya kuanza kuwapima
saratani ya matiti.
Amefafanua ugonjwa wa saratani nchini
umeshika kasi na saratani ya shingo ya kizazi ndio inayoshika nafasi ya kwanza
na nafasi ya pili ni saratani ya matiti.
Amesema kibaya zaidi idadi kubwa ya
wanaosumbuliwa na saratani hizo ni watu wenye umri chini ya miaka 60 na ipo
haja ya kuchukua hatua mbalimbali ili kuepuka ugonjwa huo.
Amefafanua ni vema wananchi wakajenga
utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ambapo
ametumia nafasi hiyo kutoa elimu ya namna ambavyo mwanamke anaweza kupima
saratani ya matiti.
“Ugonjwa wa saratani umeendelea kushika kasi
si tu Tanzania bali katika nchi mbalimbali duniani. Kwa Tanzania kwa nchi za
ukanda wa Sab Sahara inaongoza kwa saratani ya shingo ya kizazi.
“Ni ugonjwa ambao unasababisha vifo vya
mamia ya wanawake.Hivyo lazima tuchukue hatua na mojawapo ni hii ya kuhakikisha
tunatoa elimu ambayo itsaidia jamii kutambua ugonjwa na namna ya kukabiliana
nao,”amesema.
Pia amewashauri wanawake kuhakikisha
wanakuwa na mpenzi mmoja kwani kuwa na wapenzi wengi nayo husababisha kupata
saratani ya shingo ya kizazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Barclays Aron Luhanga benki hiyo imedhamiria
kuwa mstari wa mbele kuhamasisha elimu
na upimaji wa saratani ya matiti inafanyika ili kusaidia wanawake kujikinga
mapema na ugonjwa huo.
“Benki ya Barclays imeamua kushirikiana na
Tanzania Beast Cancer Foundation(TBCF) katika kuhimiza wafanyakazi kupima na
kupata elimu kuhusu ugonjwa huu ili kujua afya zao.
“Mchakato huu wa kupima na kutoa elimu
unaenda sambamba na juhudi za kutokomeza kasi ya ukuaji wa saratani ya matiti
ambayo huathiri na kuua wanawake asilimia 50,”amesema.
Amefafanua tangu mwaka 1991 kila ikifika
Oktoba hufahamika kama mwezi wa kusheherekea saratani ya matiti na hiyo ni
baada ya mwanamke Janelle Hail ambaye alikutwa na ugonjwa huo akiwa na miaka 34
na kwa wakati huo saratani ya matiti haikuwa na elimu ya kutosha wala
uhamasishaji mkubwa kwa jamii,”amesema.
Aron amesisitiza Barclays imeamua kuimarisha
utoa elimu na upimaji wa saratani ya matiti kwa lengo la kuthibitisha afya ya
mwanamke.Pia kuhakikisha wengine ambao
bado hawajapima wanachukua hatua hiyo na kujua hali ya afya zao.
“Benki ya Barclays inaendelea kuimarisha
huduma za jamii na kuweka mchango mkubwa katika kuhakikisha jamii inaendelea
kikamilifu kwa kutilia mkazo Nyanja zote zinazozunguka binadamu,”amesema.
No comments:
Post a Comment