HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 21 September 2018

DK NDUGULILE AZINDUA HUDUMA YA TB KUPITIA TEKNOLOJIA YA SIMU ZA MKONONI

Na Zanab Nyamka, Globu ya Jamii.
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt  Faustine Ndugulile amewataka Wizara ya Afya kuongeza idadi ya mikoa iliyopo katika programu ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi ili kila mwananchi aweze kupata huduma hiyo.

Hayo yamesemwa leo wakati wa uzinduzi wa huduma ya TB kupitia kupitia teknolojia ya simu za mkononi unaojulikana kama TAMBUA TB  kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kufahamu kuhusu dalili za Kifua  pamoja na mpango labambe wa kudhibiti kifua kikuu nchini.

Dkt Ndugulile amesema kuwa pamoja na kuwa na programu hiyo lazima Wizara watoe elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Kifua Kikuu ambapo inakadiriwa zaidi ya vifo 27,000 vinasababishwa na uginjwa huo.

Amesema, katika kuboresha na kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu, wameweka mifumo ya tambua ambapo imeongeza mashine 209 zinazoweza kutambua mgonjwa ndani ya masaa mawili.

Dkt Ndugulile amesema, kupitia Wizara mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma inatekeleza mpango mkakati wa miaka mitano 2015-2020 lengo likiwa ni kupunguza maambukizi mapya ya TB kwa asilimia 20 na idadi ya vifo vinavyotokana na TB kwa asilimia 35.

Amesema, kuwa kutokana na mpango wa Wizara wamewekea mkakati wa kuboresha zaidi huduma  na kutoa rai ya kuongeza idadi ya mikoa kwani wananchi wote wanahitaji huduma hiyo ili kupunguza kasi ya maambukizi.

Katika mfumo huo wa TAMBUA TB, Wizara itaweza kufanisi na ufuatiliaji na kuhakikisha kuwa taarifa zote zinakusanywa na kutumika ipasavyo ikiwemo idadi ya watu waliosajiliwa, idadi ya ujumbe uliotumwa kwa walengwa , idadi ya wateja wa TB waliogunduliwa na ufuatiliaji wa wagonjwa kwa wakati muafaka.

Meneja wa mradi Dk Beatrice Mutayoba amesema kuwa mradi huu utasaidia katika kutambua wagonjwa wa kifua kikuu kwa njia rahisi kwa kuweza kupitia ujumbe wa uchunguzi binafsi baada ya kujibu maswali kuligana na dalili za ugonjwa wa TB, na iwapo mteja ana dalili za TB mfumo utamuelekeza kwenda kwenda kwenye kituo cha huduma za afya kilicho karibu nae kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Dk Beatrice amesema, tayari wameshatoa mafunzo kwa watoa huduma 520 na watoa huduma kazi ya kujitolea 200 kutoka Mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Geita, Mwanza na Arusha kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi watakaotumia mfumo wa programu ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi.

TB inashika nafasi ya 9 kwa kusababisha vifo duniani na ni ugonwa pekee wa kuambukiza unaoongoza ukifuatiwa na VVU, na inakadiriwa kwa mwaka 2016 watu Milioni 10.4 duniani waliugua TB, Milioni 1.7 walifariki dunia wakati milioni 4.3 hawakugunduliwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya afya duniani ya Shirika la Afya kwa mwaka 2017, Tanzania imeonekana ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye wagonjwa wengi wa TB na takwimu za mpango wa taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) za mwaka 2017  zinaonesha jumla ya wagonjwa 69,818 wa TB waligunduliwa ambapo asilimia 90 walitibiwa na kupona. Hata hivyo inakadiriwa kuwa wagonjwa wanaofikiwa ni asilimia 44 ambapo kuna wagonjwa 84,000 wenye TB ambapo bado wapo kwenye jamii na wanaendelea kuambukiza.

Huduma hiyo inapatikana katika namba *152*05# kisha chagua namba 6.
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt  Faustine Ndugulile  akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi  uliojulikana kwa jimba TAMBUA TB akiwataka kuongeza  idadi ya mikoa ili wananchi wapate huduma hiyo nchini kote.
Meneja wa mradi wa ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi  Dk Beatrice Mutayoba akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo akielezea namna mfumo utakavyosaidia kutambua wagonjwa kwa njia rahisi na kwuashauri kufika katika kituo cha afya kwa ajili ya kupata matibabu.
Baadhi ya washiriki mbalimali wakiohudhuria uzinduzi wa programu ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi  uliojulikana kwa jimba TAMBUA TB.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt  Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja madaktari kutoka sehemu mbalimbali na mashirika yalityosaidia kufanikisha mradi huo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad