HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 17 September 2018

MTAMBO KUPIMA SAMPULI YA MAGONJWA YA SARATANI WAZINDULIWA

Na Khadija Seif , Globu ya jamii

WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na  Taasisi ya Madaktari nchini Marekani  inayoshughulika na magonjwa ya saratani (ASCP) wamezindua rasmi mitambo wa kupima sampuli ya vipimo  vitakavowezesha  kwa baadhi ya magonjwa kama saratani kufanyiwa ugunduzi wa haraka zaidi.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Mpoki Ulisubisya amesema leo jijini Dar es Salaam dhumuni la taasisi hiyo ni kupunguza mrundikano wa wagonjwa wengi kwa wakati mmoja.

Amefafanua kwani hapo awali vipimo hivyo vilikua vikichukua muda mrefu kupata majibu hivyo basi mtambo huo utawezesha kutoa majibu  ndani ya siku tatu na kumpatia tiba haraka mgonjwa atakaegundulika ana tatizo la saratani.

Dk.Ulisubiya ameongeza wataalam waliopo kwa sasa ni takribani 20 ambao wanataaluma ya Pathology ambao watasaidia wagonjwa wenye saratani  na hospital ambazo zimepewa vifaa hivyo ikiwamo Hospital ya Taifa Muhimbil, Ocean road na KCMC Moshi  itawasaidia wakufunzi kusoma kwa vitendo zaidi.

Kwa upande wa Daktari wa magonjwa ya saratan  Dk. Edda vuhahula ametoa shukrani za dhati kwa taasisi hiyo kwa kuleta vitendea kazi   na kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kutoa tiba haraka na kunusuru kutokana na magonjwa hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad