HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 30, 2018

MKUTANO MKUU WA WADAU WA TASNIA YA KOROSHO WAFANYIKA MTWARA


Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba akizungumza latika mkutano wa wadau wa Korosho uliofanyika mjini Mtwara. 

 Mkutano mkuu wa wadau wa Tasnia ya Korosho unefanyika  Jumamosi ya Tarehe 29 septemba2018, umeipitisha Bei Elekezi/Bei Dira kuwa ni Tsh.1550 (Daraja la Kwanza) na Tsh1240 (Daraja la 2) huku Mjengeko wa bei ukiwa ni Tsh 1696 (Daraja la kwanza) na Tsh 1386 (Daraja la pili). 

 Kwa kawaida Mnunuzi haruhusiwi kununua chini ya Bei Elekezi na hivyo kwa bei hii Kuna asilimia kubwa ya Bei kwenye minada Kupanda zaidi ya msimu uliopita, hasa ikizingatiwa kuwa Bei Elekezi kwa msimu uliopita ilikuwa 1450 (Daraja la kwanza na 1160 Daraja la Pili, lakini Wanunuzi kwenye minada walinunua hadi Tsh 4000 kwa Kilo, kwahiyo ni wazi msimu huu asilimia za bei kupanda minadani ni kubwa. 

 Bei hiyo imepitishwa kwa asilimia mia moja na wajumbe wa mkutano huo, baada ya mapendekezo ya kamati yaliyowasilishwa kwa kuzingatia tafiti zilizofanyika.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha mapendekezo ya kamati kwa wadau, Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Korosho Tanzania amesema Kamati hiyo imejumuisha uwakilishi wa wajumbe kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo Naliendele, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, vyama vikuu vya ushirika, washauri wa kilimo, warajisi wasaidizi wa Mikoa, wakulima kutoka mikoa inayolima zao korosho kwa wingi, pamoja na bodi ya korosho Tanzania. 

 Awali akifungua mkutano huo mgeni rasmi ambaye ni waziri wa kilimo Dr.Charles Tizeba amesema korosho ni zao la kwanza kuliingizia taifa fedha za kigeni na ni zao la kimkakati na kuwataka wakulima kuzipuuza taarifa za kwamba msimu huu bei itashuka. 

 “Korosho inachukua namba moja kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni, hatukuwahi kupata mnunuzi wa marekani lakini safari hii wapo,mmoja anataka tani elf 70 na wapo wanunuzi wa kutoka nchi nyingine kibao..Sasa nyie endeleeni kupiga maneno korosho haina bei wakati wenzenu tunasonga mbele!” ~ Amesema Waziri Tizeba
Licha ya uwepo Waziri Tizeba, mkutano umehudhuriwa pia Omary Mkumba, naibu waziri kilimo, Anna Abdalla ambaye ni mwenyekiti wa Bodi , Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya korosho, Mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania, Mwakilishi wa Katibu mkuu wizara ya fedha na mwakilishi wa katibu mkuu wizara ya kilimo, Wabunge wa mikoa inayolima korosho, Wakulima, Wabanguaji wakubwa na wadogo wa korosho, Wasambazaji wa pembejeo korosho Mwenyekiti wa chama cha wanunuzi wa korosho na wadau mbalimbali wa kilimo kama Ansaf na wengine. 

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Mama Anna Abdalla amesema kumekuwa na songombingo ya walanguzi wanaosambaza taarifa za uongo ili kuwahujumu wakulima. “Naomba wakulima wa korosho wauze korosho kwenye mfumo rasmi na wapuuze songombingo za kuendeleza kangomba zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii ..Wanasema bei itakuwa chini,..Bei Dira imechelewa, sijui mkutano wa wadau hautokuwepo..WAPUUZENI na kuhusu Suala la Korosho kukutwa na kokoto limetutia doa na kwa hakika serikali imechukua hatua ingawa siwezi kuzitaja hapa. Bodi ina Akiba ya sulphur zaidi ya tani elf 10..Wakulima watunze fedha wanunue wakati wa minada/ mauzo waweke Akiba Majumbani” Amesema Mama Anna Abdallah (Mwenyekiti Bodi Korosho).

Aidha taarifa iliyotolewa na Ofisa uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana, imesema tarehe rasmi ya kufunguliwa kwa msimu na kuanza kwa minada vitatangazwa Kesho Jumapili Sept 30, kwenye mkutano kati ya CBT na wanahabari utakaofanyika kwenye ofisi za bodi hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad