HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 30 September 2018

MATUKIO KATIKA PICHA: MECHI YA SIMBA NA YANGA ILIYOPIGWA JIONI HII UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR


Beki wa Timu ya Simba, Pascal Wawa akiwania mpira wa juu na Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Heritier Makambo, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliowakutanisha watani hao wa jadi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. timu hizo zimetoka sare ya ya 0-0.  

Na Agness Francis,Globu ya jamii
MTANANGE wa Watani uliokuwa  unasuburiwa  wa watani wa  jadi Simba na Yanga wametoshana mguvu kwa kutoka sare ya  bila kufungana Katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wa timu hizo kwa shauku uliweza kumalizika kwa suluhu ya Kutokufungana katika dakika zote 90.
Katika kipindi cha Kwanza kilianza kwa  kukamiana kwa Kila upande  kushambulia lango la mwenzake kutafuta matokeo mazuri ya kuongoza ambapambo kila timu ilicheza Kwa kujituma.

Mpaka dakika 45 za  Mpira zimemalizika wachezaji Wakienda mapumzikoni matokeo yalikuwa 0-0

Kipindi cha pili kilianza  kwa kukamiana yanga walionekana kuzidiwa nguvu kwa kushambuliwa  lango lake  kwa mashuti ambayo hayakuleta madhara kwao.

Mpira ulikuwa wa kasi kila mmoja aliitaji matokeo ya ushindi dhidi ya mwenzake na mpaka dakila 90 zimemalizika hakuna lango lililoona lango la mwezie.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa Deus Kaseka na Ibrahim Ajibu wamepotea mchezoni kwa sababu ya kuwabadilishia staili ya kucheza lakini pia amefurahishwa na matokeo hayo ya Leo.

Amesema, Simba ilikuwa na presha ya kutufunga tulijua hilo mapema na ndio manaa tukawaachia mpira wacheze wao sisi kazi yetu ilikuwa ni kuzuia"amesema Zahera.

Ligi kuu Tanzania bara (TPL)Imesimama yanga akiwa nyuma ya mbao FC kwa alama 13  akiwa amecheza mechi 5, simba huku simba ana pointi 11,kupisha maandalizi ya kikosi  cha Taifa stars kinachoingia leo kambini  kwa ajili ya kujiandaa na mchezo Dhidi ya Cape Verde michuano ya kufuzu Kombe la Afcon yatakayofanyika mwakani nchini  Cameroon. 
 Mgeni rasmi katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akiwa ameongozana na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakwembe pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinzia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakiingia uwanjani kwa ukaguzi wa vikosi hivyo, kabla ya kuanza kwa mchezo, uliopigwa jioni ya leo kwenye Dimba ya Taifa, jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa sare ya 0-0.
 Kikosi cha Timu ya Yanga kilichoanza leo.
 Kikosi cha Timu ya Simba kilichoanza leo.

 Kiungo wa Yanga, Abdallah Haji akiondosha hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni kwake na Mshambuliaji wa Simba, Mediie Kagere, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliowakutanisha watani hao wa jadi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. timu hizo zimetoka sare ya ya 0-0.  
Mlinda mlango wa Timu ya Yanga, Beno Kakolanya akicheza moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake na Mshambuliaji wa timu ya Simba, Mediie Kagere, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliowakutanisha watani hao wa jadi, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. timu hizo zimetoka sare ya ya 0-0.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad