HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 8, 2018

Mavunde aipongeza Kampuni ya Mafuta Puma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakiwasaidia kuvuka kwenye kivuko wanafunzi wa shule za msingi za Upanga na Maktaba mara baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Trafiki akisikmamisha magari ili kurughusu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakiwasaidia kuvuka kwenye kivuko wanafunzi wa shule za msingi za Upanga na Maktaba mara baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakipiga picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa shule za msingi za Upanga na Maktaba mara baada ya hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti wakikabidhi mfano wa cheki yenye tahamani ya shilingi milioni tano kwa mwalimu Mkuu wa wa shule ya msingi Upanga Ailika Yahya mara baada ya shule hiyo kuibuka mshindi katika shindano hilo lililoshirikisha wanafunzi wa shule za msingi za Upanga na Maktaba katika shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde akimkabidhi zawadi za mshindi wa kwanza Mwanafunzi wa shule za msingi ya Maktaba Francisco Salvatory kwa mwakilishi wake Elisha Msafiri katika hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la uchoraji wa picha za usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa Dar es salaam kushoto ni mwalimu mkuu wa shule ya Upanga Ailika Yahya.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti pamoja na majaji wengine wakichambua picha za wanafunzi walioshinda katika shindano hilo. Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde akizungumza katika hafla hiyo kushoto aliyekaa ni Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Upanga wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Mavunde. Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Maktaba wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Mavunde.




NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde, ameipongeza Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, kwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kujali usalama wa wanafunzi kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya uchoraji kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa huo.Amesema tangu mwaka 2013, kampuni hiyo ilipoanzisha kampeni ya usalama barabarani ambayo imekuwa na lengo la kupunguza ajali za usalama barabani na sasa mafanikio yanaonekana.

“Tangu ilipozinduliwa kampeni hii tunaona kuna mafanikio na katika awamu ya kwanza ya mafunzo haya wanafunzi 9,152, wamepewa mafunzo usalama barabarani ikiwamo kushiriki katika michoro hongereni sana Puma.
“….na la kufurahisha zaidi ni hatua ya kuzishirikisha na shule za wanafunzi wenye ulemavu ikiwamo ya shule mojawapo ya Mkoani Ruvuma,” amesema Mavunde.

Awali Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuwaelimisha wanafunzi kuhusu usalama barabarani tangu mwaka 2013 ilipozinduliwa kampeni hiyo.“Tangu ilipoanza kampeni hii tumetoa mafunzo kwa wanafunzi wapatao 68,000 katika shule 63 za mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Geita, Kilimanjaro na Ruvuma,” amesema .

Alisema madhumuni ya kuwahusisha wanafunzi wa shule za msingi imetokana na kuamini kwamba mafunzo ya salama barabarani yanatakiwa kutolewa kwa watto wadogo ili waweze kukua wakiwa na uelewa kuhusu usalama barabarani.
“Tumeamua kuweka mkazo katika mafunzo haya kwa wanafunzi tukielewa kuwa wanakabiliwa na hatari nyingi za barabarani. Na kuyafanya mafunzo haya kuwa kipaumbele chetu cha kwanza,” amesema Philippe.

Meneja huyo alisema kuwa kwa mwaka huu wamefundisha wanafunzi 9,152 wa shule za msingi 16 za Mkoa wa Dar es Salaam na Ruvuma pamoja na kuendesha mafunzo hayo kwa shule za walemavu na kuwa kampuni ya kwanza ya mafuta kuendesha mafunzo hayo.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliibuka mwanafunzi Francisco Salvatory wa Shule ya Msingi Upanga ambaye alinyakua kitita cha Sh 500,000 wa pili ni Magreth Andrew wa Shule ya Msingi Maktaba, ambaye alivyakua kitita cha Sh 300,000 na wa tatu ni pia alikuwa mwanafunzi wa shule ya Msingi Upanga ambaye alizwadiwa Sh 150,000 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad