HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 26 September 2018

MAANDALIZI YA FIBA ZONE 5 YAKAMILIKA, MASHINDANO KUANZA SEPT 30

 Rais wa TBF Phares Magessa akizungumza  na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya maandalizi ya mashindano yanayoandaliwa na shirikisho la mpira wakikapu duniani kwa ukanda wa Africa yajulikanayo kama “FIBA ZONE V CLUB CHAMPIONSHIP”.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Shirikisho la Mpira wa kikapu nchini (TBF) limekamilisha maandalizi ya mashindano yanayoandaliwa na shirikisho la mpira wakikapu duniani kwa ukanda wa Africa yajulikanayo kama “FIBA ZONE V CLUB CHAMPIONSHIP”.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa juma moja kuanzia tarehe 30 Septemba mpaka 08 Octoba 2018 mwaka huu katika Uwanja wa Ndani wa Taifa na  uwanja wa Bandari Kurasini.

 Akizungumzia maandalzi pamoja na ufunguzi wa mashindano hayo, Rais wa TBF Phares Magessa amesema kuwa Mashindano hayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na kufungwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harisson Mwakyembe.

 Mashindano haya yatahusisha jumla ya nchi 9 ikiwemo wenyeji  Tanzania, Kenya, Uganda , Rwanda , Burundi , Sudan Kusini, Misri , Somalia na Ethiopia na jumla ya timu 21 kutoka kwenye nchi hizo za  wanaume zikiwa 14 na wanawake 7 zitashiriki mashindao hayo.

Magessa amesema kuwa mashindano haya yana tija kubwa sana kwa sabau timu zitapata uzoefu kutoka kwa timu zingine kutoka nchi za Afrika na Tanzania watawakilishwa na timu na 3 JKT na Oilers za wanaume na JKT wanawake.

Mashindano haya yatajumlisha nchi 9 kutoka ukanda wa tano huku timu 3 zikiwa hashiriki, timu hizo ni Uganda, Ethiopia, Kenya,  Somalia, Rwanda, Burundi, Misri na, Sudan Kusini pamoja na wenyeji Tanzania.

 Pia sambamba na mashindano haya kutakuwa kuna michuano ya kutafuta bingwa wa 3x3 kwa timu za Taifa kutoka nchi 9 za ukanda wa 5  na bingwa ataenda kuwakilisha ukanda huu katika mashindano ya Afrika ya 3x3 . 

Magessa amewaomba Wadau kushirikiana na TBF  kufanikisha michuano hii wakiwa ado wanahitaji wafadhili ili kufanikisha mashindano haya.

Timu zitaanza kuwasili kuanzia tarehe 28-09-2018  kwa timu za Kenya , Rwanda na Ethiopia huku  Shirikisho linapenda kuwakaribisha kuja kujionea msisimko wa michuano hii na kurejesha heshima ya mchezo wa kikapu nchini.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad