Na Felix Mwagara, MOHA-Kakonko
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kigoma kuhakikisha wanawadhibiti baadhi ya askari Polisi na Uhamiaji ambao wanatabia ya kujihusisha na vitendo vya rushwa, kunyanyasa wananchi katika vizuizi pamoja na maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Lugola pia aliitaka kamati hiyo kushirikiana na vyombo vya dola mkoani humo katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa shughuli za Wizara yake anayoiongoza ni mtambuka.
Akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, Lugola alisema vyombo vya dola vifanye kazi kwa weledi na kuwezesha utekelezaji wa malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano, hasa katika kuwezesha Tanzania ya viwanda.
“Vyombo vyetu vya dola visikwamishe shughuli za watu wengine na taasisi nyingine zisitumie vyombo hivyo kukwamisha bali kuwezesha,” alisema Lugola na kuongeza kuwa;
“ Kamati hii ya Ulinzi na Usalama ya mkoa akikisheni mnawasimamia vizuri viongozi wa vyombo katika kudhibiti askari wachache wanaoharibu sifa za Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji na wengineo kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa na kunyanyasa wananchi,” alisema Lugola.
Aidha, Waziri Lugola aliwataka askari wa usalama barabarani wasimamie sheria na wawe wakali na wasitishwe na mtu ila wasionee wananchi.
Lugola, pia aliwataka Makamanda wa Mkoa huo wahakikishe magari yanakaguliwa, madereva wanapimwa vilevi na askari wa usalama barabarani wawe wakali katika kusimamia sheria bila kuangalia cheo wala wala hadhi ya mtu ila akasisitiza wasionee mtu.
Waziri Lugola ameanza ziara yake ya kutembelea mikoa yote nchini kwa kuanzia Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.
Kaimu
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kakonko, Mkoa wa Kigoma, Julius Samwel,
akimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto)
Jengo la Wilaya hiyo, alipowasili wilayani humo kwa ajili ya ziara ya
kikazi. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Simon Mando.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akizungumza na
Wajumbe wa Kamati yaUlinzi na Usalama ya Wilaya ya Kakonko (upande wa
kushoto) pamoja na Kamati ya Mkoa (upande wa kulia) katika Ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo, leo. Lugola aliwataka wajumbe hao
kuwadhibiti baadhi ya askari Polisi na Uhamiaji ambao wanatabia ya
kuomba rushwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo katika vizuizi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Kaimu
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kakonko, Mkoani Kigoma, Julius Samwel
(kushoto) alipokua anatoa taarifa ya Wilaya ya Ulinzi na Usalama katika
Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, leo. Lugola aliwataka
wajumbe wa Kamati hiyo pamoja naya Mkoa huo kuwadhibiti baadhi ya askari
Polisi na Uhamiaji ambao wanatabia ya kuomba rushwa katika maeneo
mbalimbali yakiwemo katika vizuizi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (aliyeshika kitabu) akitoka
katika ofisi ya Wilaya ya Kakonko, Mkoani Kigoma, akielekea katika
Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kwa ajili ya kufanya kikao na
Wajumbe wa Kamati yaUlinzi na Usalama ya Wilaya ya Kakonko pamoja na
Kamati ya Mkoa, leo. Katika kikao hicho, Waziri Lugola aliwataka wajumbe
hao kuwadhibiti baadhi ya askari Polisi na Uhamiaji ambao wanatabia ya
kuomba rushwa katika maeneo mbalimbali yakiwemo katika vizuizi. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment