HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 7, 2018

KUIONA SIMBA NA AFC LEOPARDS BUKU TANO TU KESHO UWANJA WA TAIFA.

Afisa habari wa Simba Haji Manara. 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
TIMU ya Simba inashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na AFC Leopards ya Kenya kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea tena wiki ijayo utakaochezwa kesho katika dimba la uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mchezo huo, Afisa habari wa Simba Haji MAnara amesema katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa wa klabu ya Simba na AFC Leopards ya Kenya utakaofanyika Jumamosi kiingilio kitakuwa ni Sh. 5,000 kwa majukwaa ya mzunguko.

Manara ametaja viingilio vingine katika mchezo huo utakaoanza Saa 12:00 jioni vitakuwa Sh. 15,000 kwa jukwaa la VIP A na Sh. 10,000 kwa jukwaa la VIP B na mchezo huo utakuwa ni kwa ajili ya kuwapima wachezaji wake kabla ya kuendelea na mtanange wa ligi kuu.

Amesema mchezo huo utazikutanisha timu hizo baada ya miaka miwili toka wakutane mara ya mwisho kwenye tamasha la Simba Day, Agosti 8 mwaka 2016 Uwanja wa Taifa pia na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa golo 4-0.

Mbali na hilo, Manara amewataka mashabiki wa Simba na watanzania wote kwa ujumla kuipa sapoti Taifa Stars ambayo inacheza kesho dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kufuzu kuelekea AFCON 2019.

Manara amesema watanzania kwa ujumla wanatakiwa kuwa wamoja kwa ajili tawashangaa mashabiki baadhi wa Simba ambao wataipa sapoti Uganda kutokana na kuondolewa kwa wachezaji wake 6 kwenye kikosi cha Stars kutokana na kuchelewa kufika kambini akieleza kuwa ni sababu ambayo haina maana.


Manara amewaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa kesho ambapo timu yao itakuwa inacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya majira ya saa 12 jioni.

Sanjari na kujitokeza Uwanjani, mashabiki hao pia ambao watawahi watapata fursa ya kuutazama mchezo wa Uganda dhidi ya Stars ambao utarushwa mbashara kupitia kituo cha ZBC 2.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad