HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 8, 2018

KAMPUNI YA KITANZANIA YA NALA YASHINDA TUZO YA ECOBANK FINTECH CHALLENGE

SHINDANO la Ecobank Fintech Challenge lenye lengo la  kuonesha na kushirikiana na  miradi yenye mafanikio zaidi ya Fintech Katika bara zima la Afrika limemalizika huku Tanzania kupitia Kampuni ya Nala kupitia mradi wake wa Nala Money(Nala App) chini ya Mkurugenzi na mwanzilishi Benjamin Fernandes wakiibuka na kuwa washindi,

Shindano hilo limelenga  kusaidia kupitia ushirika wa kibiashara ili kukua na kujitanua kwenda kwenye mafanikio ya kikanda na biashara ya kimataifa.

Mradi wa malipo ujulikanao kama Nala hapa Tanzania umetajwa kuwa mshindi wa mwaka wa shindano hilo la Ecobank Fintech Challenge na kufanikiwa kuibuka na zawadi ya dola za kimarekani 10,000.

Nala inawasaidia watumiaji wa miamala ya simu kujihusisha na nakala za USSD kupitia njia rahisi kama vile Venmo app, iliyotoa ufumbuzi pamoja na miradi (startups) mingine ipatayo 10 katika sherehe za 30 agosti katika makao makuu ya kimataifa ya Ecobank huko Lome Togo.
Nigeria wallet, imekuwa ya pili na kujishindia dola za kimarekani 7,000 wakati Virtual Identity ya Afrika ya Kusini ilikuwa mshindi wa tatu na kupata dola za kimarekani 5,000. Washiriki wengine ni Lypa ya Kenya, Litee ya Benin, SESO Global ya Afrika ya Kusini, InvestED  ya Sierra Leone, Eversend ya Ufaransa, Seca pay ya Nigeria, Moji pay ya Togo na Awamo ya Uganda.

Ecobank itawaandikisha washindi wote 11 katika ushirika wake wa Fintech. Ushirika huu utadumu kwa kipindi ya miezi 6. Katika kipindi hicho miradi hiyo (startups) itanufaika kutoka kwenye fursa hiyo  kwenda kwenye hatua kubwa Zaidi ya ushirika na Ecobank Group.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu(kushoto) akimpongeza Mkurugenzi na mwanzilishi wa Kampuni ya  Nala, Benjamin Fernandes baada ya kuibuka mshindi wa Tuzo ya Ecobank Fintech challenge.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad