HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 28 September 2018

JUKWAA LA MAARIFA NA TAARIFA ZA AFYA LAZINDULIWA NCHINI


Na Avila Kakingo,Globu ya jamii
JUKWAA la maarifa na taarifa za afya lazinduliwa na TanzMED jijini Dar es Salaam leo.

Jukwaa hilo litakuwa kwa mfumo wa application (programu ya simu) ya simu ya mkononi inayopatikana kwenye toleo la Android pekee pamoja na tovuti ya www.tanzmed.co.tz yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa taarifa na maarifa ya afya Tanzania na nchi mbalimbali wanaotumia lugha ya Kiswahili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwanzilishi mwenza wa Tanz MED Mkata Nyoni amesema lengo kuu la kuanzishwa programu hiyo ni kuhakikisha jamii inanufaika na ukuaji wa teknolojia na mtandao wa matumizi ya huduma ya simu kwa upatikanaji wa taarifa za afya popote walipo.

“Tumeamua kuanzisha mtandao huu ili kuhakikisha jamii wanakuwa na uelewa mpana wa maswala ya afya pamoja na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za afya hii ni juhudi za kuunga mkono Serikali ya viwanda kwa kuhakikisha kuwa na jamii ya watu wenye afya,"amesema.

Nyoni amesema katika Application hiyo ya jukwaa la TanzMED linawmwezesha mtumiaji kusoma makala za afya zilizoandikwa na madaktari bingwa, kusikiliza simulizi za makala za afya na kupata orodha ya vituo vya afya kama hospitali, maduka ya dawa na maabara kulingana na umbali ulipo.

 Pia amesema kuwa taarifa za chanjo kwa watoto, taarifa za kriniki na taarifa za watu wanaotumia bima za afya.

Ameongeza wanawezesha mwanamke na wasichana kufatilia taarifa za mwenendo wa siku zao za hedhi kwa kupokea ujumbe kwenye simu zao pale wanapokaribia siku zao

Huku ikimpa nafasi ya kumuunga mweza wake ambaye naye ataweza kufatilia siku za hedhi ili kuchukua maamuzi sahihi.

Ameeleza kuwa pia Application wanajamii hawataweza tena kusahau muda wa kunywa dawa na kwenda kriniki kwani TanzMED itawawakumbusha kwa kuwatumia ujumbe kwenye simu zao za mkononi.

 Mkurugenzi wa Tume ya Saansi na Teknolojia (COSTECH), Amos Nungu (wapili Kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na vijana wavumbuzi waliovumbua Application ya Afya kwa jamii inayotumia simu za mkononi. kulia ni Moja ya wavumbuzi wa Application ya jukwaa la maarifa na afya, Mkata Nyoni, na kushoto ni Mkuu wa fedha na uendeshaji DTBi Makange Mramba.
 Moja ya wavumbuzi wa Application ya jukwaa la maarifa na afya, Mkata Nyoni akizungumza na waandishi wa habari leo alipotambulisha aplication ya TanzMED jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya Saansi na Teknolojia (COSTECH), Amos Nungu.
Moja ya wavumbuzi wa Application ya jukwaa la maarifa na afya, Mkata Nyoni akionesha application ya TanzMED inavyopatikana kwenye simu ya mkononi leo katika uzinduzi jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad